Serikali nchini
Ecuador inasema kuwa idadi ya watu waliouawa kwenye tetemeko kubwa la
ardhi la siku ya Jumamosi, imeongezeka hadi zaidi ya watu 500.
Naibu
waziri wa mambo ya ndani (Diego Fuentes) ameonya kuwa idadi hiyo huenda
ikaongezeka zaidi kwa sababu waokoaji wanazidi kukosa matumaini ya
kupata manusura zaidi.Takriban watu 2000 bado hawajulikani waliko. Watu 20,000 wameachwa bila makao kufuatia tetemeko hilo la uzito wa 7.8 katika vipimo vya richa lililoikumba nchi hiyo.
Chanzo Habarileo
0 comments:
Post a Comment