Maziko ya mwili wa aliyekuwa
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus
Liyumba yatafanyika kesho mkoani Morogoro baada ya kukamilika kwa
taratibu za kuaga mwili wake leo jijini Dar es Salaam.
Liyumba alifariki dunia
juzi saa 10.00 jioni katika Hospitali ya Aga Khan kutokana na maradhi ya
kisukari na shinikizo la damu ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda
mrefu mpaka dakika ya mwisho.
Akizungumzia taratibu za mazishi, msemaji
wa familia, Moses Liyumba alisema marehemu atazikwa nyumbani kwake
Morogoro.
“Marehemu alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan siku tatu
kabla ya kufariki dunia. Bado tunaandaa utaratibu wa kuaga mwili kisha
kuelekea Morogoro kwa ajili ya maziko,” alisema Moses nyumbani kwao Kawe
Avocado.
Moses, ambaye ni mtoto mkubwa wa Liyumba, alisema marehemu
baba yake ameacha watoto saba aliozaa na mke wake aliyefariki dunia
mwaka 2005.
“Tunasikitika kwa kifo cha mzee wetu, lakini ndiyo mapenzi
ya Mungu. Watoto wake wote tupo, na wengine wawili wanaoishi nje ya nchi
wameshafika kwa ajili ya kumpumzi- sha mpendwa baba yetu.”
Mkurugenzi
huyo wa zamani wa BoT aliandikwa sana kwenye vyombo vya habari mwaka
2009 alipokuwa anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi kati ya
mwaka 2001 na 2006 wakati wa ujenzi wa majengo pacha ya makao makuu ya
BoT.
Siku ya hukumu ya kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
shtaka la kuisababishia Serikali hasara ya Sh221 bilioni lilitupwa,
lakini alitiwa hatiani kwa shtaka la matumizi mabaya ya madaraka.
Liyumba alitiwa hatiani Mei 23, 2010 kwa kosa hilo na kufungwa miaka
miwili jela mpaka Septemba 24, 2011 alipoachiwa huru.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment