Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepiga marufuku wananchi
wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara kwa kuwa wanachangia uwapo
wa watu hao huku baadhi ya watu wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato
kinyume cha sheria.
Akizungumza
jijini dar es salaam Bw.Makonda amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa la
watoto katika barabara kadhaa za jiji la dar wakijihusisha na Kuomba
pesa huku wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni jambo ambalo ni kinyume na
sheria lakini pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.
Aidha
amesema mkakati uliokuwapo kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii,
Tamisemi pamoja na manispaa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakusanywa na
kuwekwa katika vituo maalum huku wanaohusika na kuwatumia kufanya kazi
hiyo wakichukuliwa hatua.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment