Halmashauri zinazoongozwa na vyama vya upinzani nchini vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) zinakusudia kujiondoa kuwa wanachama wa Jumuiya ya Halmashauri Nchini (ALAT), endapo mapendekezo waliyoyatoa yatapuuzwa.
Akiwasilisha
maazimio ya kikao chao jana mbele ya waandishi wa habari mjini Dodoma,
Makamu Mwenyekiti wa umoja wa wenyeviti na mameya wa halmashauri
zinazoongozwa na (UKAWA) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, Bw.
Calist Lazaro, alisema wamependekeza kubalishwa kwa sheria na kanuni za
katiba ya (ALAT), ili ziweze kuendana na wakati uliopo na kutoa
mazingira rafiki kwa vyama vya upinzani, ili viweze kuwa na uwakilishi
katika kamati tendaji ya (ALAT) taifa
Ukawa,
ambayo inaundwa na vyama vya Chadema, CUF, NLD na NCCRMageuzi,
imeshikilia majiji na halmashauri kubwa nchini baada ya kupata ushindi
kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 uliokuwa na ushindani mkubwa.
Kati
ya majiji, miji na halmashauri 26 zilizo chini ya vyama hivyo, kuna
majiji matatu ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam, baadhi ya manispaa
muhimu za miji kama Iringa, Moshi na Siha mkoani Kilimanjaro, Tunduma
(Songwe), Monduli (Arusha), Kinondoni na, Ilala (Dar es Salaam).
Alisema
athari itakazopata kama wakijitoa ni kuyumba kifedha kutokana na ukweli
kuwa majiji na halmashauri hizo ndizo zinazotoa michango mikubwa kwenye
mfuko wa umoja huo.
“Kama
mambo tuliyopendekeza hayatafanyiwa kazi, tutajitoa kwenye umoja huu na
kuangalia uwezekano wa kuunda umoja mwingine ambao kweli utakuwa ni kwa
maslahi ya taasisi hizi za serikali za mitaa,” alisema.
“Halmashauri zetu hazitachangia, Alat wabaki na chombo chao.”
Mbali na michango, Alat pia hutegemea fedha za wafadhili na wadhamini wa shughuli zao.
Kalist,
ambaye ni meya wa Jiji la Arusha, aliiutaka uongozi wa Alat kufanya
marekebisho ya katiba na kanuni za Alat ziweze kuendana na wakati kwa
kutoa mazingira rafiki kwa vyama vya upinzani.
Alisema
mazingira hayo ni kuwa na uwakilishi katika kamati ya utendaji ya Alat
Taifa kama ilivyo bungeni na katika kamati za fedha za halmashauri
ambapo suala la uwepo wa uwiano wa kivyama miongoni mwa wajumbe ni la
kikanuni.
Pia
mameya na wenyeviti hao walitangaza kutoutambua uongozi mpya wa Alat
kwa madai ulichaguliwa kinyume cha Katiba ya Alat na kanuni za uchaguzi
za mwaka 2009.
“Tunaomba
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua mapato na
matumizi ya Alat kwa kuwa fedha hizi ni za wananchi zinazochangwa
kupitia halmashauri zao,” alisema.
Miongoni
mwa mambo wanayodai kukiukwa katika uchaguzi huo ni pamoja na kumruhusu
Meya wa Jiji la Tanga kugombea umakamu mwenyekiti, wakidai kuwa si
chaguo la wananchi wa jiji la Tanga kupitia madiwani wao.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment