Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein (atikati) akiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid
na Katibu wa Baraza hilo kuingia kwenye ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi, Mbweni nje ya mji wa Zanzibar kwa ajili ya kuzindua baraza hilo la tisa.
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ametangaza hatua za kubana
matumizi ya serikali yake, lakini pia akifuata nyayo za Rais John
Magufuli kwa kuahidi kukabiliana na vitendo vya rushwa kwa kutumbua
majipu ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wanyonge kuona wanafaidika na
huduma muhimu zinazotolewa na serikali.
Aidha, amesema Baraza lenye mawaziri makini na miongoni mwa majukumu
yake makubwa kuhakikisha Zanzibar inajitegemea na kupunguza utegemezi
kutoka kwa nchi washiriki wa maendeleo.
Dk Shein alisema hayo wakati akilizindua Baraza la Wawakilishi la
Tisa, ikiwa ishara ya kuanza kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba,
ikiwemo kuisimamia Serikali na kupitisha matumizi ya fedha za serikali
kwa wizara kwa ajili ya mwaka waAliwataka watendaji wa taasisi hizo,
ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Bodi ya Mapato (ZRB)
kuwa wabunifu zaidi kwa kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato na
kupambana na watu wanaokwepa kodi ikiwemo wafanyabiashara.
“Serikali zetu mbili zimeamua kubana matumizi yasiyokuwa ya lazima
ambapo sasa tutakuwa tukifuatilia zaidi katika taasisi zinazokusanya
kodi kuona kwamba watendaji wake wanakuwa makini zaidi na kuwa
wabunifu,” alisema Dk Shein aliyeshinda Uchaguzi Mkuu wa marudio wa
Machi 20, mwaka huu.
Kuhusu maadili na utawala bora, alisema atahakikisha kuanza kutumika
kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2015 ambayo
itafuatilia utendaji wa viongozi waliopewa dhamana zao kuona kwamba
wanawajibika kikamilifu kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Alisema moja ya kazi kubwa atakayoifanya katika kipindi cha miaka
mitano ni kuhakikisha Serikali inapambana na rushwa ambayo ni adui wa
haki kwa watendaji wa serikali ikiwemo viongozi waliopewa majukumu.
Alisema yapo manung’uniko makubwa kutoka kwa wananchi kwamba wapo
viongozi wanaendekeza rushwa na huduma muhimu hazipatikani bila ya kutoa
fedha na matokeo yake wananchi kuichukia Serikali yao.
‘Rushwa na vitendo vya aina hiyo ndiyo yanayoitwa
majipu.....nitahakikisha tunatumbuwa majipu na kutoa moyo wake hadi
kuhakikisha haki inatendeka kwa wanyonge kuona wanafaidika na huduma
muhimu zinazotolewa na serikali,” alisema Dk Shein na kuongeza kuwa,
“sasa imetosha.”
Alieleza kuwa malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ifikapo
mwaka 2020 kuyafikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati, utakaoongeza
ajira kwa vijana na kuweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo.
Alisema hali ya uchumi wa Zanzibar imekuwa ikitoa matumaini makubwa
kutoka ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 6.6 katika mwaka 2015, na kuwa
matarajio makubwa ni kufikia asilimia 8.10 ifikapo mwaka 2020.
K u h u s u maslahi kwa watumishi wa Serikali, alisema ahadi yake
aliyoitoa wakati wa mikutano ya kampeni ya kuongeza kima cha chini cha
mishahara ya wafanyakazi wa SMZ kufikia Sh 300,000 ipo pale pale na
ataitekeleza.
Aidha, alisema alitoa ahadi kwa wapiganaji wa vikosi ya Idara maalumu
za Serikali kuongeza viwango vya mishahara kulingana na wenzao wa
Serikali ya Muungano kwamba atazitekeleza katika mwaka wa fedha
kulingana na hali ya makusanyo ya kodi.
Hata hivyo, alisikitishwa na tatizo la wafanyakazi wengi wa SMZ
kushindwa kuwajibika ipasavyo huku wale wenye majukumu ya kutoa huduma
kwa wananchi wakiyakwepa na kupelekea wananchi kuichukia Serikali.
Alisema katika Serikali atakayounda haitovumilia wafanyakazi
watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria za utumishi
na kusema wafanyakazi wa aina hiyo watawajibishwa kwa kufukuzwa kazi.
“Hatutawavumilia wafanyakazi wa serikali waliopewa jukumu la kutoa
huduma na kushindwa kutekeleza majukumu hayo......mshahara unatokana na
jasho la kazi unayoifanya kwa hivyo wafanyakazi wazembe tutawafukuza,”
alisema Dk Shein.
Aidha, alitangaza neema kwa wakulima wa zao la karafuu zaidi katika
kisiwa cha Pemba na kusisitiza kwamba faida ya asilimia 80 wanayoipata,
itaendelea kuwepo huku wakulima hao wakipewa motisha ya kuimarisha
mashamba ya karafuu na vitalu vya miche hiyo.
Aliwakumbusha Wazanzibari kuwa uchaguzi umekwisha na kazi kubwa
iliyopo sasa ni wananchi kujenga nchi na kuimarisha umoja na mshikamano
ambao ndiyo malengo ya serikali yanayotokana na utekelezaji wa Ilani ya
CCM.
Alisema Chama Cha Mapinduzi CCM ndiyo kilichopewa ridhaa ya kuongoza
nchi kutokana na kukubalika kwa Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka
2015-2020 kwa hiyo viongozi wanatakiwa kubeba jukumu hilo kwa kufanya
kazi na kuweka pembeni itikadi za kisiasa.
Alisema ataendelea kuwa muumini wa umoja na utulivu wa Wazanzibari
wote huku akisisitiza kuwaunganisha wananchi wote wa Zanzibar kwa
kuongoza nchi bila ya chuki, jazba au uonevu kwa itikadi za kisiasa,
lakini hatamvumilia yeyote atakayeibeza Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984
akiapa kupambana naye kwa nguvu zote.
Alisema hana mbadala wa Muungano na kuahidi kushirikiana na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Magufuli kuleta
maendeleo na kupambana na umasikini wa wananchi kwa kufuata Ilani ya
CCM. fedha wa bajeti.
Alisema Serikali itachukua hatua za kubana matumizi yasiyokuwa na
lazima na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kutoka katika vyanzo vyake
na kusimamia taasisi zilizokabidhiwa jukumu hilo kuona ufanisi
unapatikana.
Chanzo HabariLeo.
Tuesday, 5 April 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment