Katika
kuelekea bunge la bajeti hivi karibuni, serikali imeshauriwa kuongeza
bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuendana na
kauli ya upatikanaji wa elimu bure sambamba na kufidia gharama za
uboreshaji na ujenzi wa miundombinu.
Kauli
hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na John Kalage Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Hakielimu, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya
uchambuzi na ushauri wa Shirika la Hakieli juu ya mwelekeo wa bajeti ya
elimu2016/2017.
Kalaghe
alisema serikali haina budi kuongeza bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka
wa fedha 2016/2017 hadi kufikia asilimia 20 ya bajeti ya taifa au
asilimia 6 ya pato lote la taiafa.
Aidha
alisema kwa mujibu wa uchambuzi walioufanya kama shirika, na kwa
kuzingatia takwimu za idadi ya wanafunzi, shule na mahitaji, kila mwaka
serikali itapaswa kutenga kiasi cha fedha kisichopungua Tsh. bilioni
1,034.5 nje ya mahitaji mengine ya kisekta ili kugharamia elimu bila
malipo.
“Tunafahamu
hivi karibuni bunge linatarajiwa kuanza vikao vyake na kama watetezi na
mdau wa upatikanaji wa elimu bora nchini, tunapendekeza kwa serikali
maeneo ambayo yanahitaji kutiliwa mkazo katika upangaji wa bajeti ya
sekta ya elimu yazingatiwe” amesema Kalage.
Akizungumzia
maeneo muhimu ambayo serikali inatakiwa kuyazingatia katika upangaji
wake wa bajeti kupitia sekta hiyo alisema ni pamoja na eneo la bajeti ya
utekelezaji wa elimu bila ada, upangaji wa bajeti ya sekta ya elimu,
bajeti ya ukaguzi na uhakiki wa ubora wa elimu, mwongozo wa sera ya mpya
ya elimu na makadirio bajeti ya sekta ya elimu 2016/2017.
Alibainisha
kuwa eneo la bajeti ya utekelezaji wa elimu bila ada, linapaswa kuanza
kutekelezwa kabla ya agizo la elimu bila ada, suala hilo lilikuwa
likitekelezwa kupitia michango ya wazazi kwa kuchangia elimu kwa
kushirikiana na serikali.
Aidha
kuhusu gharama za kufidia ada na ruzuku shuleni kwaajili ya vifaa,
gharama za mitihani na gharama za uendeshaji kwa shule za msingi na
sekondari alisema, kwa kuwa gharama hizo zilikuwa zikifanikishwa awali
kwa ushirikiano wa michango ya wazazi na serikali basi serikali inapaswa
kufidia gharama zote kwa kutenga kiasi cha sh.bilioni 161.5 katika
maeneo hayo.
Akielezea
gharama za kufidia ujenzi na miundombinu ambao nao ulikuwa ukichangiwa
na wazazi alisema serikali kufidia gharama hizo kwa kutenga bilioni 1,
438 huku kwa upande wa gharama za kufidia utoaji wa uji katika shule za
msingi na awali itenge kiasi cha sh 198.
Vile
vile kuhusu upangaji wa bajeti wa sekta ya elimu, alishauri kuwa licha
ya changamoto zilizopo katika upangaji wa matumizi katika sekta ya
elimu, serikali inatakiwa kuangalia namna ya kuweka uwiano wa bajeti ya
matumizi ya kawaida na ya maendeleo.
“Tunaona
katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wastani wa bajeti ya
maendeleo ya sekta ya elimu imekuwa kati ya asilimia 11 hadi 16 tu
wakati ile ya matumizi ya kawaida ikifikia asilimia 80 hadi 90, kihalali
kiasi kinachotengwa ni kidogosana kulinganisha na changamoto,
“Mathalani bajeti ya mwaka 2015/2016 bajeti nzima ilikuwa sh. Bilioni 3,887 huku bajeti ya maendeleo ikiwa ni asilimia 16 tu” amesema.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment