Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema katika bajeti ya
mwaka huu Serikali imepanga kununua magari mengi na kuyasambaza katika
vituo vya polisi vyenye shida ya vitendea kazi.
Kitwanga
alisema hayo bungeni jana alipokuwa akijibu swali Mbunge wa Igalula,
Musa Ntimizi (CCM), aliyetaka kujua kama wizara haioni umuhimu wa
kuvipatia vituo vya polisi magari ambavyo havina katika jimbo hilo ili
kurahisisha utendaji kazi.
Mbunge
huyo pia alitaka kujua kama Serikali itakuwa tayari kumalizia ujenzi wa
kituo cha polisi katika Kata ya Loya katika Halmashauri ya Tabora
(Uyui) ambapo kwa sasa wananchi wameishiwa nguvu ya kuendeleza ujenzi
huo.
“Serikali
inatambua kazi kubwa inayofanywa na wananchi katika kuchangia
maendeleo, naomba mbunge uwasiliane na wizara ili tuweze kuona namna ya
kusaidia kumalizia ujenzi wa kituo hicho,” alisema Kitwanga.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment