Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, ameibukia kanisani na kutoa ya moyoni, ikiwa siku tano baada ya Rais Dk. John Magufuli kutengua uteuzi wake.
Kilango,
Jumatatu wiki hii uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Machi 20, mwaka
huu, kudai kuwa mkoa wa Shinyanga hauna mtumishi hewa wa serikali hata
mmoja.
Hata
hivyo, Ikulu ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa katika taarifa za awali
kuna watumishi hewa 45, huku kazi ya uhakiki ikiendelea katika wilaya
za Ushetu na Shinyanga.
Rais
Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa wote, alipokuwa akiwaapisha kuwa
wafanya uchunguzi kuhusu uwapo wa watumishi hewa katika mikoa yao na
kutoa taarifa.
Kutokana
na kutoa taarifa hizo zisizo za kweli, Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli
alitangaza kutengua uteuzi wake, akiwa amekaa kwenye nafasi hiyo kwa
siku 27. Kilango amekuwa mkuu wa mkoa wa 19 tangu kuanzishwa kwa mkoa
huo.
Mbali
na Kilango, Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi Katibu Tawala wa Mkoa
wa Shinyanga, Abdul Dachi, kutokana na taarifa hizo za kutokuwapo
watumishi hewa katika mkoa.
Alivyosema Kanisani
Akiwasalimia
waumini wenzake juzi, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, mjini Shinyanga,
baada ya kupewa fursa ya kusema neno, Kilango alisema anamshukuru Mungu
kwa kila jambo kwa yote yaliyomtokea.
“Ndugu
waumini wenzangu, hili ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu. Hata mtu
unapojifungua mtoto akafariki dunia, unamshukuru Mungu kwani hayo ni
mapenzi ya Mungu.
"Ukiona mzazi wako kafariki dunia pia, unamshuruku Mungu. Tunao wajibu wa kumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema kwa maneno mafupi na kisha kuketi, huku akiacha simanzi miongoni mwa waumini wenzake, wakiwamo viongozi wa kanisa.
Alivyoanza Kazi
Mbele
ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), muda mfupi baada ya
kuanza kazi, Kilango alisema Shinyanga ni mkoa wenye changamto nyingi
ambazo atazishughulikia, lakini atakuwa akilazimika kukimbia Dar es
Salaam kumwona mwenzi wake, Mzee John Malecela ambaye ni mgonjwa, na
pindi hali yake ikiimarika wataungana naye mjini Shinyanga.
Hayo aliyasema Machi 22, mbele ya wajumbe wa kikao cha kamati hiyo na Ijumaa Machi 25, alisali kanisani hapo.
Sambamba
na hayo, aliahidi kupambana na watumishi wazembe na wale wanaoendekeza
rushwa na ufisadi na kurejesha hadhi ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo.
Kilango
ambaye yuko mjini Shinyanga, akisubiri kukabidhi ofisi kwa mrithi wake
kwa mujibu wa utaratibu, bado anaishi hotelini kwa vile aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa huo, Ally Rufunga, hajaondoka katika nyumba ya serikali iliyoko
Ikulu ndogo, eneo la Lubaga.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment