Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa huo.
Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.
Aidha
mkuu huyo wa mkoa alisema anafanyia kazi sakata la mkazi wa Kata ya
Ngarenaro anayedaiwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za
kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira
ya kutatanisha.
Ntibenda
alisema hayo jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za
mitaa 154, maofisa watendaji kata 25 pamoja na wenyeviti wa serikali za
mitaa.
Alisema
suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa
wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki, daladala na
wapiga debe.
Alisema
kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho nyakati za kazi, amepiga
marufuku uuzwaji wa kilevi hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua za
kisheria zitachukuliwa.
“Sitaki
kuona viroba vikiuzwa katika Mkoa wa Arusha na atakayekiuka
nitamchukulia hatua za kisheria, lakini huyu anayeuza dawa za kulevya
halafu polisi wanamwachia na wananchi hawajui kwanini anaachiwa huku
akiendelea kuuza dawa, sasa nasema mwisho wake umefika, nitafuatilia kwa
makini suala hili.”
Baadhi
ya wenyeviti wa serikali za mitaa walihoji sababu za kutokuwa na ofisi
za kufanyia kazi badala yake wanalazimika kutumia nyumba zao au
kukodisha ofisi ili kufanya kazi za jamii lakini pia hawana posho za
vikao.
Wenyeviti
hao akiwemo Amani Mwakalinga wa mtaa wa Darajani na Hilary Mkonyi wa
mtaa wa Ngarenaro, walisema awali Mkurugenzi wa Jiji, Juma Idd aliahidi
kuwajengea ofisi lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment