Facebook imeripoti
ongezeko la faida kwa asilimia 195 katika robo ya kwanza ya mwaka huku
kampuni hiyo ikiendelea kupata mapato ya matangazo mapya.
IIiripoti
mapato ya dola bilioni 1.5 katika kipindi cha kati ya mwezi Januari na
Machi ikilinganishwa na mapato ya dola milioni 512 mwaka uliopita.Mbali na kuwapatia wenye matangazo huduma mpya kama vile video, Facebook iliimarisha mauzo yake kutokana na huduma zilizopo.
Facebook pia imependekeza mpango mpya wa hisa ambao utampatia fursa mwanzilishi wake Mark Zuckerberg kuuza hisa zake bila kupoteza udhibiti wa kampuni hiyo.
Kampuni hiyo imesema kwamba hatua hiyo itampa moyo bwana Zuckerberg kusalia katika uongozi wa facebook.
Thamani ya hisa za facebook ilipanda hadi asilimia 9 baada ya kufanya biashara.
Chanzo Habarileo.
0 comments:
Post a Comment