Msako ulioanzishwa na Rais John Magufuli wa kutokomeza tatizo la wafanyakazi hewa katika utumishi wa umma, umeendelea kuibua mazito, ambapo mkoani Kilimanjaro, Benki ya CRDB imejikuta ikitoa mkopo kwa waliokuwa wafanyakazi hewa.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu aliyasema hayo akidai
kuwa, yamegundulika baada ya Serikali kuunda kamati za uchunguzi wa
tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 500 katika halmashauri hiyo.
Kabla
ya kuibuka kwa kisa hicho kinachoonesha namna wafanyakazi hewa
alivyokuwa wakiibia nchi, hivi karibuni mkoani Singida, Mhasibu wa
Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Nyamangaro, alipandishwa
kizimbani akidaiwa kujilipa mishahara ya wastaafu 57, yenye thamani ya
Sh milioni 29.4.
Mbali
na mhasibu huyo, Rais Magufuli alipokuwa mapumziko kijijini kwake
Mlimani, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, alieleza kisa kingine
kilichoshitua jamii kuwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kulikuwa na
mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17.
Benki ya CRDB Hai
Akizungumza
jana, Mchomvu alidai kuwa watumishi watatu wa halmashauri hiyo; wawili
wa Idara ya Utumishi na mmoja Mchumi, walikopa katika Benki ya CRDB Sh
milioni 35.2, kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu Idara ya Utumishi na Utawala, Gudila
Mashele, Ofisa Utumishi Daraja la Kwanza, Faraja Ndatu na Mchumi Daraja
la Pili, Isaiah Bayege.
Kutokana na tuhuma hiyo iliyoibuliwa na kamati hizo za uchunguzi, Mchomvu alisema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, limewafukuza kazi watumishi hao.
Kutokana na tuhuma hiyo iliyoibuliwa na kamati hizo za uchunguzi, Mchomvu alisema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, limewafukuza kazi watumishi hao.
Mbali
na tuhuma ya kujipatia mkopo kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa,
Mchomvu alisema kuna watumishi wengine wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za
wizi wa fedha za muda wa kazi wa ziada wa madaktari na wauguzi katika
Hospitali ya Machame wilayani hapa, huku mwingine akifukuzwa kwa kununua
dawa hewa za hospitali hiyo.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Mhasibu Daraja la Kwanza, Edwin Kalokola na
Mhasibu Msaidizi, Valentina Elisha, wanaodaiwa kuiba Sh milioni 24.4 za
muda wa kazi wa ziada wa madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo.
Mbali
na wahasibu hao, yupo pia dereva Derick Urassa, aliyefukuzwa kwa tuhuma
za kushiriki katika ununuzi wa dawa hewa katika hospitali hiyo zenye
thamani ya zaidi ya Sh milioni 32.7.
Walioshushwa cheo
Alisema wapo pia watumishi walioshushwa vyeo kutokana na tuhuma mbalimbali, ikiwemo kughushi nyaraka na kuidhinisha malipo bila idhini ya mwajiri.
Walioshushwa cheo
Alisema wapo pia watumishi walioshushwa vyeo kutokana na tuhuma mbalimbali, ikiwemo kughushi nyaraka na kuidhinisha malipo bila idhini ya mwajiri.
Miongoni
mwao ni pamoja na Ofisa Muuguzi Msaidizi Daraja la Kwanza, Agness Chami
na Katibu wa Afya Daraja la Kwanza, Gilbert Mashamba.
Wengine
ni wahasibu waandamizi wawili, Kasisim Herpa na John Bogohe na Mhasibu
Daraja la Kwanza, Christopher Manzi, ambao wanatuhumiwa kuidhinisha
malipo mbalimbali ya Sh milioni 488.2, bila kuwa na idhini kinyume na
taratibu za kazi.
Walivyobambwa
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Saidi Mderu alisema tuhuma hizo ziligunduliwa na Mkaguzi wa Ndani wa halmashauri hiyo, Michael Mosha na kufanyiwa kazi na tume hizo zilizoongozwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Saidi Mderu alisema tuhuma hizo ziligunduliwa na Mkaguzi wa Ndani wa halmashauri hiyo, Michael Mosha na kufanyiwa kazi na tume hizo zilizoongozwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli.
Baada
ya kubainika kwa tuhuma hizo, Mderu alisema baraza hilo lilimpongeza
mkaguzi huyo kwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwa kuwa angeweza
kudanganyika kutumia fedha hizo.
Mkuu
wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa, amepongeza baraza hilo kwa hatua
hizo na kueleza kuwa kazi kubwa ya madiwani ni kusimamia mali na
rasilimali za Serikali, ili wananchi wapate huduma bora za Serikali yao
ya Awamu ya Tano ambayo ina dhamira ya kuwahudumia.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment