Agizo
la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi
baada ya karandinga kuanza kuwasomba ombaomba waliojaa katika maeneo
mengi jijini hapa.
Makonda
alitangaza kuanza kuwaondoa ombaomba hao juzi, huku akipiga marufuku
wananchi kuwapa pesa kwa kuwa ndicho chanzo cha kuwapo kwao jijini hapa.
Zoezi hilo la kuwaondoa watu hao lilianza juzi usiku katika maeneo ya Mnazi Mmoja, Samora na Kariakoo.
Jana maeneo mbalimbali ambayo aghalabu ombaomba hupenda kukaa yalikuwa tupu.
Maeneo hayo ikiwamo barabara ya Morocco, Magomeni Usalama, Fire na Baridi hayakuwa na watu wa kundi hilo.
Mmoja
wa ombaomba aliyekuwa na watoto wawili alipomuona mwandishi wa habari
hizi katika maeneo ya Fire, alitimua mbio na kujificha pembeni mwa
barabara, huku akisema: “Tumetoka Dodoma, hatutaki kurudi.”
Kadhalika,
operesheni hiyo licha ya timuatimua kuwakumba ombaomba, wapigadebe nao
wameunganishwa katika kundi hilo kwa kuanza kuondolewa kwenye vituo vya
mabasi.
Baadhi
ya wapigadebe hao wamedai ni vigumu kwa Makonda kuwaondoa kwa kuwa
wanachofanya ni kwa manufaa ya maisha yao na hawana pa kwenda.
Agizo
la kutaka ombaomba wakamatwe na kuondokana na vitendo hivyo liliwahi
kutolewa pia na waliowahi kuwa wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf
Makamba, Abbas Kandoro na Said Mecky Sadiki.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment