Mtoto
George Elias (7) amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba ya katani
katika Kijiji cha Buganzu, Kata ya Uyovu wilayani Bukombe, Mkoa wa
Geita, tukio linalodaiwa kusababishwa na michezo ya kitoto.
Baba
wa mtoto huyo, Elias Martin alisema mwanawe alikuwa anasoma darasa la
awali katika shule ya msingi ya kijiji hicho na siku ya tukio alikwenda
kucheza na watoto wenzake.
Martin
alisema akiwa nyumbani kwake akipata chakula cha mchana na wageni
waliokwenda kumtembelea, walifika watoto watatu wa jirani yake wakidai
mtoto wake ananing’inia juu ya mti.
Alisema
baada ya kupokea taarifa hiyo aliambatana na wageni wake mpaka eneo la
tukio na kumkuta mtoto huyo akining’inia kwenye mti uliopo pembeni ya
nyumba yake.
Mzazi
huyo alisema chanzo cha tukio hilo ni michezo ya watoto na huenda
alidanganywa na wenzake kuweka shingo kwenye kamba walipokuwa wakicheza.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Matayo Paschal alisema kuwa alipokea taarifa ya kifo hicho na kulijulisha Jeshi la Polisi.
Kamanda
wa Polisi mkoani hapa, Mpojoli Mwabulambo alisema wamefungua jalada la
uchunguzi kuhusu tukio hilo, lengo likiwa kujua chanzo cha kifo hicho.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment