Wataalam wa maswala
ya afya wa shirika la Afya duniani WHO wanahofu kuwa virusi vinasambaa
mbali na kwa haraka,vikisababisha madhara makubwa.
maambukizi yamekuwa yakihusishwa na maelfu ya watoto wanaozaliwa wakiwa na vichwa vidogo.tahadhari ya WHO kuhusu Zika ni ya hali ya juu sawa na ya Ebola
hii inamaanisha kuwa utafiti na msaada itatolewa kwa haraka kupambana na maambukizi.
Mkurugenzi mkuu wa WHO, Margaret Chan amesema nguvu ya pamoja inahitajika kupambana na virusi hivyo
amesema masuala yanayopewa kipaumbele ni kuwalinda wanawake wajawazito na Watoto dhidi ya mbu wanaosambaza virusi.
Tangu mwezi Oktoba kumekuwa na ripoti ya kesi 4,000 za watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo nchini Brazil pekee.
Chanzo BBBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment