Tumbili.
WASHTAKIWA saba wa kesi ya kusafirisha wanyamapori hai 61 aina ya
tumbili kwenda nchini Armenia, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Moshi na kusomewa mashtaka manne likiwamo la uhujumu uchumi.
Wakiwa mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi, Joackim Tiganga, mawakili wa
serikali watatu, Wankyo Saimon na Salim Msemo, wakiongozwa na Abdalah
Chavula walieleza mahakama hiyo kwamba washtakiwa hao kwa pamoja
walikula njama ya kutenda kosa.
Wakili Saimon aliieleza mahakama hiyo kuwa shtaka la kwanza la
uhujumu uchumi linawahusu washtakiwa wote, ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi
Msaidizi Wanyamapori, Dk Charles Mulokozi na Ofisa Mfawidhi Kanda ya
Kaskazini anayehusika na matumizi endelevu ya wanyamapori nchini
(CITES), Nyangabo Musika.
Wengine ni maofisa wanyamapori, Martina Nyakangara na Very Antony,
wafanyabiashara Iddy Misanya na Artem Vardanian na wa mwisho ni Meneja
wa Hoteli ya North Sea, Eduard Vardanyan.
Alieleza mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja kati ya
Februari 1 hadi Machi 22 mwaka huu wakiwa katika mikoa ya Arusha, Dar es
Salaam na Kilimanjaro walikula njama ya kutenda kosa la kusafirisha
nyara za serikali.
Wakili Saimon akisaidiwa na wakili Msemo walisema shtaka la pili
linawahusu washtakiwa wote kwa pamoja ambapo washtakiwa wengine wakiwa
watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kutumia nyadhifa zao
walishirikiana kula njama za kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini
Armenia.
Walidai kuwa katika shtaka hilo washtakiwa hao kwa pamoja walikuwa na
njama za kusafirisha wanyama hao 61 wenye thamani ya dola za Marekani
7,320 sawa na kiasi cha Sh 15,872,029 bila kibali cha Mkurugenzi wa
Idara ya Wanyamapori.
Chanzo HabariLeo.
Friday, 1 April 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment