JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini.
Hayo
yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya
Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam jana
mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa
marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao
unaonesha umeanza kushamiri.
Kamishna
Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na kuzisajili na kufanya
malipo katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri.
Akizungumzia
vitendo vya uhalifu Mssanzya alisema kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri
kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule
wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa
“Hivi
karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali
wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji
na kufanyiwa uchunguzi” alisema Mssanzya.
Alisema
watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea
kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo
zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.
Alisema
pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako
katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na
kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao.
“Jeshi kama jeshi peke yake haliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwa, hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa,” alisema.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment