Wednesday, 9 March 2016

Tagged Under:

Trump ashinda Mississipi na Michigan

By: Unknown On: 00:17
  • Share The Gag
  • Donald Trump
    Mgombea anayeongoza katika chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amejiongezea ushawishi kama mgombea mkuu kufuatia ushindi wake katika majimbo ya Michigan na Mississippi.
    Wadadisi wanasema kuwa ushindi huo mara mbili umezima uvumi wa mwishoni mwa wiki kuwa kampeni yake Trump ilikuwa imepoteza kasi.
    Baada ya kupata ushindi huo , Trump alisema kuwa anakiongezea umaarufu chama cha Republican. Mshindani wake mkuu Seneta Ted Cruz naye alipata ushindi katika jimbo dogo la Idaho.
    Bernie Sanders na Hillary Clinton Kwenye upande wa chama cha Democratic inaripotiwa kuwa Bernie Sanders ameshinda mchujo katika jimbo la Michigan huku naye Hillary Clinton akiibuka mshindi katika jimbo la Mississipi.

    Chanzo HabariLeo.

    0 comments:

    Post a Comment