Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali umesema kuwa
walinda amani wake watano wameuawa na wengine wamejeruhiwa vibaya katika
shambulizi lililotokea katikati ya mji wa Mopti. Waathirika wanatokea
nchini Togo.Gari lao lilipatwa na moto kabla ya kukanyaga bomu la
ardhini,na kisha kulipuka.Waziri wa masuala ya kigeni nchini Mali,
Abdoulaye Diop, ametuma salam za rambirambi katika mitandao ya kijamii
kwa UN na nchi ya Togo.Vifo vyao vimekuja wakati dunia ikiadhimisha siku
yawalinda amani.Mwaka uliopita walinda amani 129 kutoka umoja wa
mataifa walipoteza maisha katika nchi 16 wanazofanyia shughuli zao.
Chanzo BBC.
Sunday, 29 May 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment