Mwanamke
mmoja anashikiliwa na polisi wilayani Bunda, mkoani Mara kwa tuhuma ya
kumuua mtoto wake kwa kipigo, baada ya kumtuhumu kumuibia Sh 8,000.
Kamanda
wa polisi mkoani Mara, Kamishina Msaidizi wa Polisi Ramadhan Ngazi juzi
alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo, lililotokea majira ya saa 11:30
jioni katika mtaa wa majengo eneo la Bunda Day mjini hapa.
Pili
Omondo (28), mkazi wa mtaa huo alimpiga kwa fimbo kichwani mtoto wake
ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Kabarimu na kumsababishia
kifo.
Alimtaja
mwanafunzi huyo kuwa ni Wakuru Rungu (9) na kwamba baada ya kipigo
hicho alimbeba na kumpeleka hospitalini, akidai kwamba amegongwa na
pikipiki na ndipo muda mfupi akapoteza maisha.
Kamanda
Ngazi alisema kuwa mtuhumiwa huyo bado anashikiliwa na polisi na
upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji ya
mwanawe.
Habari
kutoka eneo la tukio zinadai kuwa mwanamke huyo alimpiga mtoto wake kwa
kumgongesha kichwa ukutani akidai ni mwizi sugu na kwamba baadhi ya
majirani walipomzuia alidai kwamba hata kama akimuua ni mwanawe.
Katika
tukio lingine, mwanamke mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi yake
amejifungua kichanga na kukitupa pembezoni mwa barabara kuu ya
Mwanza-Musoma, katika eneo la mtaa wa Balili mjini hapa.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment