Msanii
wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye siku za karibuni ilisemekana
alipata ujauzito na kisha baadaye ujauzito huo kuharibika amefunguka na
kuonyesha bado hajakata tamaa na anaamini ipo siku na yeye atapata mtoto
kama watu wengine wanavyopata
Kupitia Account yake ya Instagram Wema Sepetu alipost picha akiwa na mama yake mzazi na kuweka maneno yalisomeka kuwa 'iko siku na mimi nitaitwa Mama', jambo
ambalo liliibua hisia za mashabiki zake na wengine kuanza kumfariji
kuwa Mungu yupo na anasikia kilio chake na wengine wakiendelea kumtia
moyo kuwa asijali kweli upo wakati na yeye atakuwa mama na kupata mtoto.
"Muombe
Mungu Wema Sepetu hata sisi wanawake wenzako tunaumia sana kuona
unatukanwa kisa mtoto, tunakuombea Mungu akujualie mtoto wako
usisemezane nao hao watu wanakuongelea vibaya" Lovenes France
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment