Sunday, 15 May 2016

Tagged Under:

Makurutu 25 wa polisi wauawa Yemen

By: Unknown On: 03:03
  • Share The Gag
  • Makurutu hao walishambuliwa walipokuwa kwenye foleni
    Maafisa wa polisi nchini Yemen wanasema takriban makurutu 25 wa polisi wameuwawa katika shambulzi la kujitolea mhanga katika mji wa Mukalla.
    Kundi la wapiganaji wa islamic state limekiri kutekeleza shambulizi hilo, lililotekelezwa wakati makurutu hao wakiwa kwenye foleni, katika makao makuu ya polisi.
    Vikosi vya serikali ya Yemen vilikomboa mji wa Mukalla kutoka kwa wapiganaji wa Al Qaeda mwezi ulopita.

    Chanzo BBC.

    0 comments:

    Post a Comment