UJENZI
wa Mradi wa Kusindika Gesi (LNG) mkoani Lindi utakaowezesha nchi kuanza
kufanya biashara ya gesi nje ya nchi umeanza baada ya jana wadau sita
wa mradi huo kukutana na kupeana elimu kabla ya mchakato mzima kuanza
wakati wowote mwaka huu.
Kwa
kutumia mradi huo, Tanzania itaanza kufanya biashara ya gesi kwa kuuza
nje ya nchi baada ya kubaini kuwa gesi iliyogundulika baharini
inayofikia kiasi cha futi za ujazo trilioni 47, ni nyingi na ikivunwa
mahitaji ya ndani hayawezi kuimaliza hivyo kulazimika kuiuza nje ya nchi
na kuongezea Taifa mapato.
Akizungumza
jana katika mkutano wa wawekezaji na serikali kupata elimu ya mradi huo
kabla ya kuundwa kwa kamati ya majadiliano ya serikali na kuingia
mkataba wa ujenzi, Mkurugenzi wa Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC), Kelvin Komba alisema wamekutanisha wadau kutoka
serikalini na wawekezaji.
Komba
alisema mkutano huo ni kuanza taratibu za awali kuwekeza na kuuza gesi
kwa kutolewa kitaalamu rasilimali hiyo kwenye visima na kufikishwa
katika mtambo huo wa LNG ambao utaigeuza kuwa kimiminika ili ifae
kuingizwa katika matangi na kusafirishwa kwa meli kwenda katika masoko
mbalimbali duniani.
Akifafanua
zaidi, alisema mtambo huo utaipooza gesi itakayovunwa mpaka nyuzi joto
sifuri na kuipooza zaidi mpaka nyuzi joto hasi 100, ndipo inakuwa
kimiminika na kufaa kusafirishwa kwenda maeneo mbalimbali duniani.
Mradi
huo mkubwa ambao haujawahi kutokea katika historia wa miradi nchini
wenye thamani inayofikia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 60 na kutoa
ajira karibu 20,000, utawezesha nchi kukua kiuchumi.
Alisema
tayari ardhi imepatikana ya hekta 2,071 kwa ajili ya mradi wa LNG huku
hekta nyingine 20,000 zinazozunguka eneo la mradi huo, zikitengwa kwa
ajili ya viwanda.
Alizitaja
kampuni sita zinazoshirikiana katika ujenzi wa mtambo huo ni TPDC, BG
Group, Ophir Energy, Statoil, Exxon Mobil na Pavilion Energy. Mradi huo
thamani yake ni kuanzia Dola za Marekani bilioni 30 mpaka bilioni 60.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment