Chiza Dastan (31), anayesadikiwa kuwa mwizi wa pikipiki amefariki dunia
Hospitali Wilaya ya Bukombe akipewa matibabu baada ya kupigwa na nyundo
kichwani wakati akijaribu kupora pikipiki.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema tukio hilo lilitokea Mei 20
saa 4.00 usiku nje ya Baa ya Geen View, Kata ya Katente wilayani Bukombe.
Mwabulambo
alisema Chiza ambaye ni mkazi wa Kilimahewa, alifariki dunia wakati
akitibiwa baada ya kujaribu kupora pikipiki ya Nassoro Tadeo aliyemkodi
kutoka mjini Ushirombo kwenda kwenye baa hiyo.
Alisema wakiwa nje ya
baa, ghafla mhalifu alianza kuongea na watu wasiojulikana kwenye simu,
mwendesha bodaboda alishtuka na kutaka kuondoka.
Mwabulambo
alisema wakati akijaribu kuondoka, Chiza alichomoa nyundo na kuanza
kumshambulia mwendesha bodaboda na kumjeruhi kichwani.
Baada ya
mwendesha bodaboda kupigwa nyundo kichwani, aliachia pikipiki na kuanza
kupambana naye akig’ang’ania nyundo huku akiomba msaada.
Chiza alipanda pikipiki ili aondoke lakini mwendesha bodaboda, alifanikiwa kumnyang’anya nyundo na kuanza kumshambulia.
“Chiza
alipoona kipigo kimezidi aliiachia pikipiki na kukimbia kusikojulikana,
mwendesha pikipiki alichukua mali yake kwenda polisi ili kuandikiwa PF3
kwa ajili ya kwenda Hospitali ya Wilaya ya Bukombe kupatiwa matibabu,”
alisema.
Mwabulambo alisema mwendesha bodaboda kupewa PF na
kwenda kutibiwa, akiwa hospitalini hapo alishtuka kuona Chiza
akifikishwa na wasamaria wema saa 8.00 usiku akiwa na jeraha kubwa
kichwani.
“Lakini kabla polisi hawajatoa PF3 walimhoji na kubaini kuwa, ndiye aliyejaribu kuiba pikipiki,” alisema Mwabulambo.
Hata
hivyo, Mwabulambo ametoa wito kwa waendesha bodaboda kuwa makini
wanapokuwa kwenye shughuli zao, hasa nyakati za usiku na kwamba
wanapomhisi mtu watoe taarifa kituo chochote cha polisi.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Mahona Kaji alisema majeruhi alipokelewa akiwa
na hali mbaya kutokana na kupondwa na kitu kizito kichwani, fuvu la
kichwa lilionekana limepasuka. Dk Kaji alisema walijitahidi kuokoa
maisha yake lakini ikashindikana.
Credit; Mpekuzi Blog
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
ReplyDeleteKAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.