Bunge la Ugiriki limeidhinisha marekebisho kadhaa ya kiuchumi na fedha baada ya mjadala mkali wa dharura uliochukua siku nne.
Bunge limepitisha uamuzi huo, katika hatua zake kali zinazoendelea kuchukua, kuokoa uchumi wa nchi hiyo.Waziri mkuu Alexis Tsipras amesema matokeo yanaonesha kuwa Ugiriki inaheshimu ahadi zake kiuchumi.
Hata hivyo Maelfu ya waandamanaji waliandamana nje ya bunge kupinga hatua hizo zilizochukuliwa.
Mapema mwezi huu, wabunge pia walipitisha mabadiliko katika pensheni na mfumo wa kodi ya mapato.
Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment