Rais Dk John Magufuli. |
RAIS John Magufuli amemteua Gerson Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, Uchumi. Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Rais Ikulu, Dar es Salaam ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi ilieleza kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.
Kabla ya uteuzi huo, Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri na Profesa Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm). Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Tulia Ackson, aliyechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Chanzo HabariLeo
0 comments:
Post a Comment