Sunday, 15 May 2016

Tagged Under:

31 wauawa kwa bomu:Yemen

By: Unknown On: 22:17
  • Share The Gag
  • Bomu laua 31 Yemen
    Watu 31 wameuawa kwa bomu la kujitoa muhanga nchini Yemen,shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Islamic state.
    Polisi wamethibitisha kutoka kwa shambulizi hilo katika ngome iliyoko kusini mwa nchi hiyo ya Mukalla.
    Vyanzo kutoka idara ya afya vinasema kuwa zaidi ya watu sita wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.
    Maafisa wanasema kiongozi mmoja wa ulinzi na usalama alilengwa katika shambulizi la pili,ambapo aliponea chupuchupu, lakini walinzi wake wapatao sita waliuawa.
    Mashambulizi haya yanakuja pakiwa panafanyika mzungumzo ya amani kati ya serikali ya Yemeni na waasi wa Houthi yanayojaribu kuamaliza mgogoro wa zaidi ya mwaka mmoja.

    Chanzo BBC.

    0 comments:

    Post a Comment