Makamu
wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wakuu wa mikoa na wilaya
kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma wanapotaka kuwafukuza
watumishi wasio waadilifu.
Alisema
hajapinga kauli ya Rais John Magufuli ya kutumbua majipu kama
alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, hivi karibuni kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.
Samia
aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini
Arusha, wakati akisisitiza zoezi la kuhamisha mifugo iliyopo ndani ya
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa).
Alisema
wakuu wa mikoa na wilaya nchini, wanapaswa kuhakikisha wanapotaka
kuwawajibisha watumishi wa umma wanafuata sheria, kanuni na taratibu za
utumishi wa umma.
Aliongeza
kuwa mwenye mamlaka ya kutumbua majipu ni Rais pekee, kwa sababu
anateua, anaajiri na kufukuza kwa hiyo viongozi wengine wakiwamo wakuu
wa mikoa na wa wilaya wafuate taratibu.
“Rais
pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuteua, kutengua na kuajiri lakini
sijapinga utumbuaji majipu, bali nasisitiza kila mkuu wa mkoa na DC
(mkuu wa wilaya) afuate sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma,” alisema Samia.
Makamu wa Rais, aliwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha mifugo ya nje ya nchi iliyopo hifadhini inaondolewa ifikapo Juni 30.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela alishukuru Tanapa kwa kuwapa msaada madawati ili kupunguza kero ya wanafunzi kukaa chini.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera alisisitiza kuwa atahakikisha mkoa
wake unapunguza migogoro ya ardhi ili hifadhi za Taifa ziweze kulindwa,
huku wananchi wakiheshimu na kulinda mipaka ya hifadhi na rasilimali za
Taifa.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment