ASKARI
Polisi Ezekiel Dinoso (32) mkazi wa tarafa ya Mgeta, wilayani Mvomero
mkoani Morogoro amekutwa na noti bandia za Sh 10,000 zenye thamani ya Sh
870,000, akijiandaa kuzitumbukiza katika akaunti ya mtandao wa Tigo
Pesa katika duka mojawapo eneo la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema jana kuwa tukio hilo
ni la Mei 14, mwaka huu saa 1:00 usiku katika eneo la Mawezi , Manispaa
ya Morogoro.
Mtuhumiwa
alikutwa katika duka la Hadija Hamis (35) mkazi wa Chamwino, wakati
alipohitaji kuwekewa fedha hizo, mwenye duka alimtilia shaka hivyo
kuarifu Polisi.
Mtuhumiwa alipokamatwa na askari baada ya kutolewa taarifa Kituo cha Polisi, alikutwa akiwa na noti bandia 87 za Sh 10,000.
Alitaja
namba za noti hizo ni BX 7287490 zikiwa noti 22 , BX 728792 zikiwa noti
20, BX 728791 noti 19 na BX7287487 zikiwa noti 15 na kufanya jumla ya
thamani ya Sh 870,000 ambazo ni bandia.
Kamanda Matei alisema mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani.
Katika
tukio jingine, Rashidi Shabani (30) na Michael Lukasa (39), wote wakazi
wa Ngerengere wanashikiliwa na Polisi kwa kuwakuta na nyama ya nyati
kilo 300 na silaha aina ya gobole iliyotumika kumuulia mnyama huyo.
Kamanda
wa Polisi wa Morogoro, Matei, alisema walikamatwa Mei 14, mwaka huu saa
2:00 usiku katika kijiji cha Kinonko, kata ya Gwata, wilaya ya
Morogoro.
Matei
alisema, kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jitihada
zinazofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi katika kukomesha
vitendo vya uhalifu.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment