Mwanafunzi wa Chuo cha Anga (Skua) cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo Kange jijini Tanga, Philip Fred (28) amejiua kwa kujipiga risasi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul aliwaambia waandishi wa habari
ofisini kwake jana kwamba tukio hilo ni la jana saa 1.15 usiku katika
chuo hicho kilichopo kata ya Maweni nje kidogo ya jiji.
Alisema askari mwenye cheo cha Koplo mwenye namba MT 81627 alijiua wakati akiwa katika eneo la lindo chuoni hapo.
“Kimsingi
chanzo cha kifo cha askari jeshi huyo bado hakijajulikana na
imefahamika kwamba alikuwa ni mwanafunzi wa ‘Level one’ chuoni hapo na
mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Bombo”, alisema Kamanda.
Katika
tukio jingine Kamanda alisema askari wanamshikilia mkazi wa mtaa wa
Mgwisha, kata ya Pongwe jijini Tanga, Masudi Hamis (22) kwa tuhuma za
kukutwa na sare moja ya askari wa JWTZ.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment