Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko mengine ya baadhi ya
Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia maombi ya baadhi ya
Wabunge pamoja na mahitaji mapya yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa
shughuli za Kamati za Bunge.
Kwa
mujibu wa taarifa yake, mabadiliko hayo yamefanywa kwa mujibu wa Kanuni
ya 116(3) na (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili 2016
ambapo yamehusisha maeneo manne ikiwemo; Kuhamishwa kwa baadhi ya
wajumbe wa Kamati, Kualikwa kwa baadhi ya wajumbe katika Kamati ya
Bajeti, Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Haki, Maadili, na Madaraka ya
Bunge kuondolewa pamoja na Uteuzi wa wajumbe wapya katika kamati ya
Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge.
Mabadiliko
hayo ya wajumbe kwenye kamati yanaanza mara moja ambapo orodha ya
wajumbe waliobadilishwa kamati na nafasi zao ni kama ifuatavyo; Wajumbe
wanaohamishwa Kamati ni pamoja na Mhe. Ezekiel Magoyo Maige, (Mb) ambaye
alikuwa katika Kamati ya Nishati na Madini na kwa sasa anahamia Kamati
ya PAC, Mhe. Allan Joseph Kiula (Mb) ambaye alikuwa katika Kamati ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na kwa sasa anahamia Kamati ya PAC, Mhe.
Omary Tebweta Mgumba (Mb) ambaye alikuwa katika Kamati ya Sheria Ndigi
na kwa sasa anahamia Kamati ya PAC, Mhe. Rhoda Rdward Kunchela (Mb)
ambaye alikuwa katika Kamati ya Masuala ya UKIMWI na kwa sasa anahamia
Kamati ya PAC.
Wengine
ni Mhe. Joseph George Kakunda (Mb) ambaye alikuwa katika Kamati ya PIC
na kwa sasa anahamia Kamati ya PAC, Mhe. Ahmed Ally Salum (Mb) ambaye
alikuwa katika Kamati ya PAC na kwa sasa anahamia Kamati ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii, Mhe. Neema William Mgaya (Mb) ambaye alikuwa katika
Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na kwa sasa anahamia Kamati ya
Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na Mhe. Salma Mohamed Mwassa (Mb)
ambaye alikuwa katika Kamati ya Bajeti na kwa sasa anahamia Kamati ya
Ardhi, Maliasili na Utalii.
Taarifa
inaeleza kuwa, Wajumbe waalikwa katika Kamati ni pamoja na Mhe. Andrew
John Chenge (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya Sheria Ndogo, Mhe. Joseph
Roman Selasini (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya LAAC, Mhe. Dkt. Dalali
Peter Kafumu (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya Viwanda, Biashara na
Mazingira, Mhe. Japhet Ngalilonga Hasunga (Mb) ambaye yupo katika Kamati
ya PAC, Mhe. Albert Obama Ntabaliba (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya
PIC pamoja na Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Aidha,
Walioondolewa katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ni
pamoja na Mhe. Dkt. Haji Hussein Mponda (Mb) pamoja na Mhe. Najma
Murtaza Giga, (Mb).
Wanaoteuliwa
kuwa Wajumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka Ya Bunge ni pamoja
na Mhe. Asha Abdalla Juma (Mb). Mhe. Emmanuel Mwakasaka (Mb) pamoja na
Mhe. Augustino Manyanda Masele (Mb).
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment