Kipa wa timu ya taifa ya Cameroon upande
wa wanawake ameaga dunia baada ya kuzirai wakati wa mazoezi, Shirikisho
la soka la Cameroon limesema.Jeanine Christelle
Djomnang,mwenye umri wa miaka 26, aliuguwa kabla ya mechi ya Femina
Stars Ebolowa kusini mwa Cameroon Jumapili na alifariki akipelekwa
hospitalini.
Shirikisho hilo linasema taarifa za awali
zinaashiria alikufa kutokanana mshtuko wa moyo lakini sasa linasubiri
taarifa rasmi ya madaktari.
Kifo chake kinajiri baada ya mchezaji wa Cameroon Patrick Ekeng kufariki Romania.
Djomnang
alilalamika kuhisi uchungu kifuani alipokuwa akijitayarisha kwa mechi
dhidi ya Louves MINPROFF Yaounde na alikimbizwa hospitali.
Mshindi
wa tuzo ya mwanasoka bora mwanamke Afrika raia wa Cameroon Gaelle
Enganamouit, ambaye sasa anachezea timu ya Sweden, ni mojawapo ya watu
wa kwanza kussikitishwa na habari hizo.
"Ni kwa huzuni mwingi
nimepata kusikia kuhusu kifo cha mchezaji mwenzangu Djomnang Jeanine
Christelle wa Femina Stars Ebolowa, Mungu ailaze roho yake kwa amani,"
aliandika katika mtandao wa kijamii.
Kitabu cha rambi rambi kimewekwa katika makao makuu ya shirikisho la soka Cameroon kumkumbuka Ekeng na Djomanang.
Chanzo BBC.
Monday, 9 May 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment