Rais wa Marekani
Barack Obama ameelezea mikakati yake ya kubuni uhusiano thabiti na wa
kudumu na Vietnam, siku moja tu baada ya kuliondolea taifa hilo la
zamani la kikomunisti vikwazo vya silaha.
Mataifa hayo mawili
yamekuwa yakihasimiana kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa vita baridi
na uvamizi wa Marekani miaka ya sabini.Katika hotuba aliyoitoa katika mji mkuu Hanoi, Bwana Obama alisema kuwa kuboresha uhusiano wa kidiplomasia , miongo minne baada ya vita vya Vietnam, ni mfano bora wa uwiano.
Chanzo BBC
0 comments:
Post a Comment