Afisa wa usalama wa
Marekani amempiga risasi na kumjeruhi mwanamume mmoja aliyeonekana
amebeba bunduki nje ya Ikulu ya White House.
Maafisa wa Usalama
wamesema kuwa mtu huyo alielekea kwenye mojawapo wa milango ya kuingia
katika Ikulu huku amebeba silaha hiyo. Alipoamriwa aiweke chini silaha
hiyo chini akakaidi.Watu walizuiliwa kukaribia Ikulu hiyo ya White House kwa muda, huku maafisa wa Usalama wakikimbia kuhakikisha kuwa Makamu wa Rais Joe Biden, aliyekuwa katika jengo hilo wakati huo, alikuwa salama.
Rais Obama alikuwa ameondoka kwenda kucheza mpira wa gofu.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa walisikia mlio wa risasi na kisha wakamwona mwanamume mmoja mzungu akianguka chini.
Chanzo BBC>
0 comments:
Post a Comment