Mwanamke mmoja amefariki na zaidi ya wanafunzi 20 kujeruhiwa katika oparesheni ya kuiga shambulio la kigaidi ilioendeshwa
nchni kenya, katika chuo kikuu cha Strathmore.Oparesheni hii ilipangwa na chuo hicho pamoja maafisa wa polisi bila kuarifu wanafunzi na wafanyakazi, ili kubaini ikiwa chuo hicho kiko tayari kukabiliana na tukio la kigaidi.
Kauli rasmi kutoka chuo kikuu cha strathmore, imedhibitisha kwamba mfanyakazi mmoja amefariki kutokana na majeraha aliyopata baada ya kuruka kutoka ghorofa ya tatu
Wanafunzi zaidi ya ishirini wamejeruhiwa wanne kati yao wakiwa hali mahututi baada ya mkanyagano
mkanyangano huo ulisababishwa na mkakati wa usalama uliokuwa ukiendeshwa chuoni humo na vikosi vya usalama
Wengi waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitalini jijini Nairobi akiwemo mhadhiri aliyeruka kutoka ghorofa ya nne
waliumia miguu na mikono katika harakati za kuruka kupitia madirisha na milango wakati wa tukio hilo.
Mkakati huo ulipaswa kuangazia maandalizi ya wanafunzi na watu wengine endapo tukio la kigaidia linaweza tokea.
Hata hivyo usimamizi wa chuo hicho umeelezea kusikitishwa na jinsi tukio hilo lilivyozuka na kusababisha majeraha huku ukiahidi kuwalipia gharama za hospitali za wote waliojeruhiwa.
Tukio hili linajiri miezi kadhaa baada ya wapiganaji wa al shabaab kutekeleza shambulio la kigaidi mwezi aprili katika chuo kikuu cha Garrissa, na kusababisha vifo vya wanafunzi mia moja arobaini na saba.
Created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment