Daktari aliyewaambukiza wagonjwa 200 virusi vya ukimwi nchini Cambodia amehukumiwa jela.
Daktari
huyo bandia alipatikana na hatia ya kuwaambukiza takriban watu 200
virusi vya ugonjwa wa Ukimwi amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa
makosa yake.Baadhi ya wahasiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia.
Yem Chrin alikuwa akitumia sindano zilizokuwa zimekwisha tumika kuwatibu wenyeji wa kijiji cha Roka bila ya kujua alickuwa akisambaza Virusi vya Ukimwi.
Awali Chrin alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji lakini upande wa mashtaka ukabadilisha shtaka na kuwa kuua bila ya kukusudia.
Kesi hiyo imefichua uhaba wa madaktari na ugumu ulioko kwa raia kupata huduma za afya katika maeneo mengi ya vijijini nchini Cambodia.
Utafiti umebaini kuwa zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini huendeshwa na madakatari bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa.
Created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment