Rais wa Uturuki
Recep Tayyip Erdogan alimshawishi mwanamume, aliyetaka kujiua kwa
kujirusha kutoka kwa daraja, kubadilisha nia yake na kutojiua, afisi
yake imesema.
Mwanamume huyo alikuwa amepanga juu ya uzio wa
daraja la Bosphorus, linalounganisha Ulaya na bara Asia na alikuwa
anatishia kujiua.Msafara wa magari ya Bw Erdogan ulikuwa unapita kwenye daraja hilo mjini Istanbul wakati huo.
Picha zilizoonyeshwa kwenye televisheni zilionyesha wahudumu wa Bw Erdogan wakimsihi mwanamume huyo aliyekuwa akitokwa na machozi kuzungumza na rais.
Mwanamume huyo alitembea hadi kwenye gari la rais huyo na wakazungumza.
Baada ya muda mfupi, alisindikizwa kutoka eneo hilo.
Mwanamume huyo alikuwa akitatizwa na msongo wa mawazo kutokana na matatizo ya kifamilia, na polisi walikuwa wamejaribu kumzuia asijirushe kwa saa mbili bila mafanikio, shirika la habari la Dogan limeripoti.
Afisa wa afisi ya rais huyo ameambia shirika la habari la Associated Press kwamba kiongozi huyo aliahidi kumsaidia.
0 comments:
Post a Comment