Rais wa Urusi
Vladimir Putin kwa mara nyingine ameishutumu Uturuki kwa kudungua ndege
yake ya kivita karibu na mpaka wa Syria na kuwa serikali yake inapanga
kuiwekea vikwazo zaidi.
Katika hotuba yake ya kila mwaka bungeni,
Putin amesema hatahusisha mikakati za kijeshi dhidi ya Uturuki, lakini
amekariri kuwa uturuki ilifanya kitendo cha uhalify mkubwa.Amesema Uturuki itakuwa imepoteza mwelekeo ikiwa itadhani kuwa ni marufuku ya uuzaji wa nyanya tu ndio utakaopigwa marufuku.
Vladimir Putin ameitahadharisha Uturuki kuwa itajuta kwa kuidungua ndege ya Urusi aina ya Su-24 katika anga ya Syria.
Aliwamiminia sifa wajane wa wanajeshi wawili waliofariki baada ya shambulizi hilo.
Wajane hao walikuwa miongoni mwa wageni waheshimiwa.
Kabla ya kikao hicho kuanza wote walinyaza kimya kwa dakika moja kwa heshima ya watu 224 walikufa kufuatia ajali ya ndege kwenye rasi ya sinai nchini Misri.
Yamkini ndege hiyo ya Urusi ilidunguliwa na bomu lililotegwa ndani ya kasha la mizigo tarehe 31 Oktoba.
''Ninaamini Allah anajua ukweli uko wapi na kwanini uongozi wa uturuki uliamua kuidungua ndege yetu.''
''Bila shaka Allah amewaadhibu kwa kuwanyima busara viongozi wa Uturuki''
Created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment