NYOTA wa Bongo Fleva, Kassim Mganga, amesema kabla hajaanza kufanya
muziki alikuwa mfanyakazi wa kupokea na kutoa mizigo kwenye bandari ya
Dar es Salaam, lakini kipaji chake cha muziki kilimwachisha kazi hiyo
kutokana na ujira mkubwa aliokuwa akipata kupitia muziki wake.
Kassim alisema kwa mwezi alikuwa akilipwa Sh 200,000 kwa kazi ya
bandarini lakini katika onyesho lake moja la muziki alipata Sh 500,000
ndipo akaamua kuacha kazi ya bandari na kuendelea na muziki.
“Nilipofanya wimbo wangu wa kwanza wa ‘Haiwezekani’ nilipata shoo ya
kwanza iliyoniwezesha kupata laki tano fedha ambazo ziliniongezea nguvu
ya kufanya muziki kwa kuwa niliona mabadiliko makubwa kati ya kazi za
watu na muziki wangu,” alieleza Kassim katika uamuzi wake huo.
Created by Gazeti la Mtanzania.
Thursday, 3 December 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment