Mpango
wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Magufuli, kupunguza
matumizi yasiyo ya lazima ili fedha zitumike kuboresha huduma za jamii,
umetua kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao sasa
wameondolewa malipo ya posho wakati wanapokuwa katika vikao vya kamati
zao mbalimbali za kisekta.
Kwa
muda mrefu sasa, imezoeleka kwa wabunge kupokea posho kutoka kwenye
mashirika na taasisi mbalimbali za umma wanapoketi kutekeleza wajibu wao
ndani ya kamati za Bunge.
Hata
hivyo, posho hizo hazitakuwapo tena baada ya Msajili wa Hazina,
Lawrance Mafuru, kutangaza jana kuwa sasa posho hizo hazitatolewa tena
kwani wanachokifanya wabunge ni sehemu ya kazi zao.
Msajili
alitoa agizo hilo wakati wa mkutano wake na wakuu wa taasisi na
mashirika ya umma na pia wenyeviti wa bodi zao. Msajili Mafuru alisema
agizo hilo limetoka kwa Rais Magufuli, na kwamba sasa kinachotakiwa ni
kuona utekelezaji wake.
Bodi zafutiwa Posho za Vikao
Kadhalika,
Mafuru alisema serikali imefuta posho za mikutano ya bodi ambazo
wamekuwa wakilipwa wajumbe na kuagiza kwamba badala yake, kuanzia sasa
watakuwa wakilipwa malipo ya bodi peke (board fees), huku maelekezo
mengine yakitaka vikao hivyo vya bodi vipunguzwe kutoka kufanyika karibu
kila mwezi na sasa vya idadi ya juu vibaki kuwa vinne pekee kwa mwaka.
“Kuna
mambo ya hospitality allowances (posho za takrima). Tumepata taarifa
kwamba wabunge wanapofanya kazi za kamati, huwa wanalipwa fedha na
Bunge. Hivyo kuwapa pesa tena ni double invoice… tunahitaji kuacha
hii,” alisema Mafuru.
Alisema
zipo taarifa kwamba kuna tatizo la baadhi ya wabunge kuwa katika katika
bodi zaidi ya moja na kwamba, utaratibu huo siyo mzuri na unaweza
kuathiri utendaji kazi.
“Kuna
wakati mwingine unakuta mtu mwingine anakaa kwenye bodi hata tano au
saba. Sasa inapotokea anatakiwa kuwajibika katika bodi nyingine, anakuwa
hawezi kutekeleza wajibu wake kwavile anakuwa amebanwa na ratiba. Ila
tunashukuru kwamba sasa hivi kuna effort (jitihada) nzuri zimefanyika
kwa kuruhusu kumuondoa mbunge kwenye bodi,” alisema.
Kadhalika,
Mafuru alifichua kuwa baadhi ya Bodi za mashirika na taasisi za umma
husafiri na kundi la wabunge kwenda nje ya nchi, lakini mwishowe wabunge
hao huwa hawafiki eneo la tukio linalowapeleka nje.
“Unakuta
baadhi ya bodi zinasafiri na kundi la wabunge, halafu tunasikia wengine
hawafiki eneo la tukio. Kama ni mbinu ya kutaka wabunge wafichefiche
madudu, sidhani kama wabunge wa sasa wananunulika. Mtaenda nao huko nje,
lakini wakirudi ndani watawalipua tu,” alisema Mafuru.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment