Filamu ya ucheshi
kuhusu mkutano wa kwanza wa kuchumbiana kati ya Barack Obama na
Michelle ni miongoni mwa filamu ambazo zitaonyeshwa kwenye maonyesho ya
filamu ya Sundance 2016.
Filamu hiyo kwa jina Southside With You
inaigiza yaliyojiri adhuhuri moja majira ya joto 1989 pale Obama
alipomchumbia mkewe wa baadaye Michelle Robinson, mjini Chicago.Filamu nyingine zitakazoonyeshwa ni Swiss Army Man, ambapo mwigizaji mashuhuri Daniel Radcliffe anaigiza kama maiti.
Makala ya 2016 ya maonyesho ya Sundance yatafanyika 21 hadi 31 Januari katika Park City, Utah.
Maonyesho hayo yaliasisiwa na mwigizaji Robert Redford.
Tika Sumpter anaigiza Michelle naye Parker Sawyers Bw Obama.
Created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment