Watanzania wa Kada mbalimbali wamempongeza Rais John Magufuli kwa kuokoa mamilioni ya shilingi ambayo yangetumika kwenye maazimisho ya miaka 54 ya uhuru wa Tanzania .
Mwenyekiti
wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia
Muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, amesema kuwa uamuzi wa Rais Magufuli
wa kufuta sherehe za uhuru utakuwa umeleta tija kubwa kwa taifa ambapo
miaka mingi taifa limekuwa likichezea mabilioni ya shilingi bila faida
kwa taifa.
Mtei
amesema kuwa sherehe hizo zilizokuwa zikifanyika kwa shamrashara
zilikuwa zinagharimu fedha za walipa kodi kwa anasa za kula,kunywa na
kulewa huku watanzania wakikosa huduma muhimu.
Aliyekuwa
mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba
ameshauri kuwa sherehe hizo zifanyeke mara moja kila baada ya miaka
mitano ambapo zisihusishe matumizi mabaya ya fedha za wananchi kama
zilivyokuwa za awamu iliyopita kwa kufanya shughuli mbalimbali za
kijamii.
Naye
spika wa kwanza wa Bunge la Tanzania Pius Msekwa amesema kuwa kitendo
hicho kinapaswa kuungwa mkono kwa kila ambaye anayeitakia mema Tanzania.
Sherehe hizo jana zimewaunganisha waatanzania wote kwa kufanya jambo moja ambapo sherehe hizo zilikuwa zikifanyika Dar es Salaam pekee kwa gharama kubwa lakini jana zilikuwa za nchi nzima na zenye maslahi na taifa.
Sherehe hizo jana zimewaunganisha waatanzania wote kwa kufanya jambo moja ambapo sherehe hizo zilikuwa zikifanyika Dar es Salaam pekee kwa gharama kubwa lakini jana zilikuwa za nchi nzima na zenye maslahi na taifa.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment