Waendesha mashtaka
nchini Marekani wametangaza mashtaka mapya dhidi ya maafisa wapatao kumi
na sita wa shirikisho la kandanda duniani FIFA kwa kuhusika na tuhuma
za rushwa baada ya uchunguzi ndani ya shirikisho hilo.
Walioshtakiwa
ni pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wa Kamati ya uongozi wanaoongoza
hivi sasa na wale waliostaafu akiwemo Rais wa chama cha soka cha
Honduras Rafael Callejas.Mwanasheria Mkuu nchini Marekani Loretta Lynch amesema katika miongo miwili maafisa hao waliokula njama ya kula rushwa ndani ya shirikisho hilo ya dolla za kimarekani milioni mia mbili.
"Baraza la wazee wa mahakama wa Brooklyn wamerudisha mashtaka 92 katika Mashtaka makuuu dhidi ya washtakiwa wapya 16 wote ni maafisa wa sasa na wa zamani wa shirikisho la soka duniani. Kila mmoja katika hao maafisa 16 wameshtakiwa kwa kula njama ya kujipatia fedha kwa udanganyifu, na makosa mengine kwa kutumia nafasi zao kujinufaisha kifedha."
Aidha amefafanua kiwango cha rushwa walichopokea ni ufisadi wa kiwango cha juu.
"Sasa acha nisema uvunjifu wa uaminifu hapa ni ufisadi wa hali ya juu na kiwango cha rushwa wanachotuhumiwa hapa ni wa kupitiliza.
Na ujumbe katika tangazo hili uwe wazi kwa kila mtuhumiwa aliyebaki ambapo tumewahifadhi wakidhani wanaweza kukwepa uchunguzi huu unaoendelea, hatuwakusubiri na wala hawatakwepa lengo letu."
Aidha Kwa upande mwingine, shirikisho hilo la soka duniani limesema litaendelea kushirikiana na mamlaka nchini Marekani ambapo limetangaza mlolongo wa mageuzi ndani ya shirikisho hilo.
Created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment