Viongozi wa makanisa mbalimbali nchini, wametoa salamu za Sikukuu ya Krismasi jana, wakielezea kufurahishwa na kasi ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli.
Wamesisitiza waumini wao, kumuombea Rais na kuwataka wananchi kutii mamlaka, kwa kuwa yamewekwa na Mungu.
Viongozi
hao pia, wamewataka watendaji wa Serikali na wananchi walioshiriki
ukwepaji kodi, watubu dhambi zao na kurejesha vyote walivyochukua,
ambavyo si halali yao.
Pia, wamempa moyo Rais Magufuli kuendelea kutumbua majipu, kwani hata Bibilia inatambua kazi hiyo.
Mbali
na ujumbe huo wa viongozi wa dini kwa waumini wao na kwa Watanzania kwa
ujumla, Rais Magufuli mwenyewe alishiriki katika ibada ya sikukuu hiyo
katika Kanisa la Mtakatifu Petro, jijini Dar es Salaam, ambapo
aliwatakia Watanzania wote Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya na kusisitiza
waendelee kumuombea yeye na viongozi wengine.
Baada
ya kuwatakia sikukuu njema Watanzania, Rais Magufuli aliwakumbusha
wananchi kwamba ustawi wa nchi, unatokana na watu kufanya kazi, hivyo
baada ya shamrashamra za msimu wa sikukuu, warejee kufanya kazi kwa
bidii kwa ujenzi wa Taifa.
Dodoma wamuombea
Mkoani
Dodoma katika shamrashamra hizo, Askofu Amos Kinyunyu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Dodoma, aliwataka
Watanzania kuzidi kumuombea Rais Magufuli kutokana na utendaji kazi
unaowagusa Watanzania wa hali ya chini.
Alisema
wao kama Kanisa, wataendelea kumuombea ili afanye kazi anayoendelea
kufanya sasa hivi, kwani hata vitabu vitakatifu, vinataka usawa katika
uchumi na kipato kwa kila mtu.
‘’Tunawaomba
Watanzania wazidi kumuombea Rais wetu kasi aliyonayo aendelee kuwa
nayo, kwani Mungu anapenda haki katika maisha pamoja na uchumi ulio
sawa.
‘’Wakati mwingine hii kauli ya Hapa Kazi Tu, inakuwa hata sisi inatuogopesha, lakini Mungu ataendelea kumlinda na kumwongoza,’’ alisema.
Ni jibu la Kanisa
Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assembles of God la Miyuji Dodoma,
Samson Mkuyi alisema utawala wa Rais Magufuli, unaonekana ni jibu la
Watanzania wengi pamoja na Kanisa.
Mchungaji
Mkuyi alisema wamefurahishwa na utendaji kazi wake hasa upande wa
maadili, ikizingatiwa kuwa Kanisa linataka maadili ya kiroho na kimwili.
‘’Tulianza
kuomba haya miaka mitano, sisi Kanisa tunamwambia asiogope kwani Mungu
yupo pamoja na yeye, tunaendelea kumuombea ili Mungu aendelee kumpa
ulinzi,’’ alisema.
Atumbue zaidi
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika, Dk Dickson Chilongani alisema; ”Rais
ameonekana kutumbua majipu yaliyokuwa yamejificha na katika hili
tutaendelea kumuombea ili ayatumbue zaidi, pia na kuwafanya watendaji
wafanye kazi kwa usahihi,’’ alisema.
Rais amepatikana
Kanisa la KKKT Dayosisi ya Morogoro mbali na kurejea umuhimu wa kumuombea Dk Magufuli, liliwataka viongozi wote walioteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali, wajitoe kikamilifu kuwatumikia na kuwahudumia wananchi wakiweka mbele maslahi ya taifa.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Jacob Paulo ole Mameo, wakati wa mahubiri yake alitaka vyama vyote vya siasa, kutanguliza maslahi ya Taifa mbele na kusema mwito wa Kanisa ni sasa tusonge mbele, uchaguzi umemalizika na Rais amepatikana.

“
Rais wetu ameanza kazi yake vizuri na sasa tumuunge mkono ,
tushirikiane kwa misingi ya umoja, upendo na amani katika kujenga Taifa
na tuliombee lisonge mbele.
“Wale viongozi waliozoea kutenda uovu sasa waache, wasijiingize tena huko, tunataka wawe mfano mzuri katika kuonesha uadilifu wao kwa kusimamia huduma bora mbele ya jamii,” alisema Askofu Mameo.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude, yeye alisisitiza waumini kuhubiri upendo na kudumisha amani iliyopo.

Alipongeza
Serikali ya Awamu ya Tano, kwa hatua zake za kuwajali watu wanyonge,
ili wapate huduma bora za kijamii ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu,
uadilifu na utendaji unaozingatia sheria za nchi.
Wakwepa kodi watubu
Katika Kanisa la KKKT Usharika wa Maili Moja Kibaha, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Isai Ntele, aliwataka watu waliokuwa wakijihusisha na ukwepaji kodi hapa nchini, kutubu mbele za Mungu na kurejesha kile walichokwepa na kuonesha utii kwa mamlaka iliyopo madarakani, kwani imewekwa na Mungu.

Ntele alisema Mungu alisikiliza kilio cha Watanzania kwa kuwapa
kiongozi ambaye ana uchungu na wananchi wake, kwani ameonesha dhahiri
kuwa hataki haki za wanyonge, zipotee kwa kudhulumiwa na wachache.
“Hata Biblia inasema kila mtu aitii mamlaka iliyo Kuu kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo nimeaminiwa na Mungu, hivyo asiye na mamlaka asipotii, anashindana na agizo la Mungu hivyo watapata hukumu,” alisema.

Wanatufananisha na mbinguni
Mkoani Shinyanga, Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu, alisisitiza umuhimu wa kumwombea Rais Magufuli aliyeonesha nia ya kuwatumikia wananchi bila upendeleo, ambaye ameonesha wazi wazi kuwa anamtanguliza Mwenyezi Mungu.
"Kuna baadhi ya watu wanataka kutusadikisha kuwa Tanzania hakuna amani kwa nia zao wenyewe, labda wakilinganisha Tanzania na mbinguni ni sawa, kwa sababu mbinguni kuna utimilifu wake wote, lakini ukilinganisha Tanzania na mataifa mengine, ndugu zangu tuna amani ambayo tunapaswa kuilinda kwa nguvu zetu zote.

“Wapo
wengi wangetamani tuchinjane hapa nchini, wana wivu na chuki na nchi
yetu na pengine wanaweza hata kutumia viongozi mbalimbali kupenyeza
mambo yao, ili tuchukiane sisi kwa sisi, tuwakemee watu wanaodharau hii
amani iliyopo,” alisema Askofu Sangu.
Alisema Tanzania hata bomu likilipuka, watu wanakimbia kwenda kutazama, lakini kwa nchi zenye machafuko, likilipuka bomu hakuna anayekwenda pale kwa kuhofia kifo na hiyo ni dalili tosha kuwa kuna amani.

Askofu
Sangu aliwataka Watanzania kusherehekea sikukuu kwa upendo hususani
katika ngazi ya familia na kuhamasisha watu kuishi kwa kupendana na
kuepuka vitendo vya kupeana ujumbe wa kujengeana chuki, kwani ndiyo
chanzo cha vurugu katika jamii na taifa kwa ujumla.
Dar na mabadiliko ya kweli
Mkoani Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alisema mabadiliko ya kweli yanaletwa na watu ambao wako tayari kufanya kazi kwa dhati usiku na mchana na si matajiri.

Akitoa
mahubiri yake kwa waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph
lililoko Posta jijini Dar es Salaam, katika Ibada ya usiku wa Mkesha wa
Sikukuu ya Krismasi, alisema katika fikra za mabadiliko, watu wa kawaida
waliaminishwa kwamba hawana mchango wanaoweza kuutoa katika
mabadiliko.
“Mara nyingi sisi watu wa kawaida tulisadikishwa kwamba hakuna mchango tunaoweza kuutoa ili kuleta mabadiliko katika jumuia yetu, tulisadikishwa kwamba watu wanaokuwa na fedha na mali nyingi hao ndio wanaoweza kuleta mabadiliko katika jumuiya yetu,” alisema Pengo.

sasa mawazo hayo yamekwishatambuliwa kuwa hayakuwa sahihi, kwani watu
wenye mali si wanaoweza kuleta mabadiliko yanayotakiwa katika jumuiya ya
watu.
“Watakaoleta mabadiliko ni wale ambao haidhuru nafasi yao ni ipi katika jumuiya, lakini wako tayari kufanya kazi usiku na mchana, ili kuhakikisha kwamba hali ya kibinadamu inakuwa nzuri zaidi na huo ndio ujumbe unaopaswa kupokelewa kutoka kwa malaika aliowaendea wachungaji na kuwaambia msiogope,” alisema Pengo.

Pengo alisema na kupitia ujumbe huo wa malaika, Tanzania inaambiwa
usiogope, kwani unayo habari njema, ambayo ni kuwa tayari kufanya kila
linalokuwa ndani ya uwezo wake ili hiyo habari njema iifikie.
Aliwataka Watanzania wamuombe Mungu awajaalie neema ya kutambua kila mmoja anaweza kuwa chimbuko la habari njema na mabadiliko, si tu katika mazingira ya imani ya kidini, lakini katika mazingira hata ya kiuchumi na kisiasa.

watu hawapaswi kuogopa, bali kulinda makundi yao wakisubiri habari
njema na habari hiyo si kwa ajili ya matajiri wanaoishi katika majumba
ya kifahari, bali kwa ajili ya wote, habari ambayo ni ya furaha ambayo
ni chimbuko la heri kwa wanadamu wote.
“Habari hii siyo kwa ajili ya matajiri, siyo kwa ajili ya wale wanaoishi katika majumba ya kifalme ni habari ya furaha ambayo itakuwa chimbuko la furaha na heri kwa wanadamu wote, Mwenyezi Mungu atujaaliye hilo katika Taifa letu,” alisema Pengo.

Magufuli asisitiza kazi
Wakati viongozi wa dini wakihamasisha Watanzania kumuombea, Rais Magufuli mwenyewe alihudhuria ibada ya Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro, lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika ibada hiyo, alipewa nafasi ya kutoa salamu, ambapo aliwatakiwa Watanzania wote sikukuu njema ya Krismasi na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani wakikumbuka kufanya kazi baada ya shamrashamra za sikukuu.

Rais
Magufuli alisema watu wakumbuke kwamba ustawi wa nchi unatokana na watu
kufanya kazi ndio maana anasimamia kaulimbiu yake ya Hapa Kazi Tu.
“Tunaposherehekea sikukuu hizi, tukumbuke ya kwamba baada ya shamrashamra ni kufanya kazi kwa bidii kwa ujenzi wa Taifa letu,” alisema Rais Magufuli.

Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment