WAZIRI Mkuu Kassimu M Majaliw (pichani) kesho ataanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kigoma.
Akizungumza
na waandishi wa habari juu ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali
Mstaafu Issa Machibya alisema kuwa Waziri Mkuu atawasili Mkoani hapa
kesho majira ya saa tatu asubuhi.
Alisema kuwa atapokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Mkoa na kisha atasomewa taarifa ya Mkoa.
Baada
ya hapo ataelekea katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo
Wilayani Kasulu pamoja na kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani
Kibondo
Na
siku ya jumatatu atafungua mwalo wa kibirizi na kufanya majumuisho ya
ziara yake katika ukumbi wa NSSF na kisha kurejea Dar es salaam.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment