Wafanyibiashara
wakubwa wametakwa kuwa miongoni mwa watu wafisadi zaidi sawa na maafisa
wa polisi Barani Afrika. Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa
na shirika la kuchunguza ufisadi duniani "Transparency International".
Ni
mara ya kwanza wafanyibiashara wametajwa kuwa mafisadi wakubwa Barani.
Shirika hili limeongeza kwamba utumizi mbaya wa mamlaka unasababisha
ongezeko la umasikini, na kuwanyima raia mahitaji muhimu.Watu wengi ambao ni masikini wamejipata mara kadhaa wakilazimika kulipa hongo ikilinganishwa na matajiri, inasema "Transparency International".
Nchi ya Liberia imetajwa kama inayoongoza kwa visa vya ufisadi Afrika. Inafuatwa na Cameroon, Nigeria na Sierra leone.
Afrika mashariki Uganda inaongoza kwa visa vya ufisadi, ikifuatwa na Kenya. Kusini mwa Afrika Zimbabwe na Zambia zinaongoza katika nchi zenye visa vingi vya ufisadi.
Botswana, Mauritius na Cape Verde, ndiyo mataifa pekee ya Afrika ambapo visa vya ufisadi ni vya chini zaidi ikiwa ni asili mia mbili pekee.
Created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment