MAKAMPUNI
15 yaliyokwepa kodi baada ya kutorosha makontena yao, yamejisalimisha
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini yameshindwa kulipa kodi ndani
ya siku saba za msamaha wa Rais John Magufuli.
Kodi
inayodaiwa kwa kampuni hizo ni Sh bilioni 3.75, hivyo watachukuliwa
hatua za kisheria kwa kukwepa kulipa kodi, ikiwa ni pamoja na kufikishwa
mahakamani.
Kaimu
Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Philip Mpango alisema hayo jana wakati
akielezea makusanyo ya kodi ya makontena yaliyoondolewa katika bandari
kavu ya Azam, kinyume cha sheria pamoja na kumalizika kwa siku saba
alizotoa Rais Magufuli kwa wafanyabiashara hao kulipa kodi waliyokwepa,
bila kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
Dk
Mpango alisema siku hizo saba zimefikia kikomo juzi, hivyo hatua kali
za kisheria kwa wafanyabiashara ambao hawakulipa kodi katika kipindi
hicho zinafuata hivyo wasubiri cha moto.
“Tumewasihi
waje kulipa kwani huruma ya Rais sasa imeisha... tulifanya uhakiki na
kuthibitisha kuwa kampuni hizo zipo. Wamekuja kulalamika lakini hakika
hakuna atakayesamehewa kulipa na sasa tunafuata mkondo wa sheria ili
kuwafikisha mahakamani,” alisisitiza.
Wadaiwa
Alitaja
kampuni hizo kuwa ni Ahmed Saleh Tawred anayedaiwa Sh milioni 59.23;
Cla Tokyo Limited Sh milioni 77.52; Farida Abdullah Salem Sh milioni
75.33 na Juma Kassem Abdul Sh milioni 190.18.
Wengine
ni Libas Fashion Sh milioni 52.94; Rushy Wheel Tyre Center Co Ltd, Sh
bilioni 1.8; Said Ahmad Hamdan Sh milioni 68.36; Said Ahmed Said Sh
milioni 68.73 na Salum Continental Co Ltd Sh milioni 151.17.
Pia
yumo Salum Link Tyres Sh milioni 343.44; Simbo Yonah Kimaro, Sh milioni
69.22; Snow Leopard Building Material Co Ltd Sh milioni 93.97; Swaleh
Mohamed Swaleh Sh milioni 34.68; Tybat Trading Co Limited, Sh milioni
598.69 na Nasir Saleh Mazrui Sh milioni 70.10.
Alisema
mpaka kufikia jana TRA walikuwa wamekusanya Sh bilioni
10,643.004,948.46 kutoka kwa kampuni 28 ambapo kampuni 13 zimelipa kodi
yote iliyokadiriwa, ambayo ni Sh 4,167,130,173.89 na Sh 2,303,637,554.57
kutoka kampuni 15 zilizolipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa.
Dk
Mpango alisema Sh bilioni 4.17 zimelipwa na kampuni ya Azam ICD, ikiwa
ni dhamana ya kodi iliyokwepwa, hivyo atatakiwa kumaliza kulipa kodi
yote inayodaiwa kwa mujibu wa nafasi yake kama mwenye dhamana.
Alisema
wakati utekelezaji huo ukiendelea, ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi
hiyo ya makontena yaliyoondolewa bandarini kinyume cha sheria na
taratibu za forodha, TRA imefungua akaunti maalumu katika Benki Kuu
yenye namba 9921169785 inayoitwa Commissioner for Customs and Excise –
Container Account.
Kwa
mujibu wa Dk Mpango, mpaka sasa watumishi 36 wa TRA wanaotuhumiwa
kushiriki katika upotevu wa kodi kutokana na makontena hayo kuondoshwa
bandarini.
Watumishi wachongewa
Aidha,
alisema TRA imepata taarifa zisizopungua 15 kutoka kwa wananchi kuhusu
mali za kifisadi na mwenendo mbaya wa baadhi ya watumishi na walipakodi
wanaokwepa kodi.
Aliwashukuru
wananchi waliotoa taarifa na kuwaomba wengine wajitokeze kutoa taarifa
zaidi na mamlaka hiyo inawahakikishia kuwa itawalinda.
Dk
Mpango alisema wanaendelea kutekeleza maagizo ya Rais katika ukusanyaji
wa mapato, ikiwa ni pamoja na kupiga picha makontena yote badala ya
sampuli ya kontena ilivyo sasa na wanafanya utaratibu wa kupata mashine
za kupiga picha za nyongeza.
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment