Aliyekuwa
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) kwa miaka mitano iliyopita,
David Kafulila ameamriwa na Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora kulipa Sh7.5
milioni kama dhamana, ili ombi lake lakutaka itengue matokeo ya ubunge
wa jimbo hilo yasikilizwe.
Mahakama
imetoa uamuzi huo kupitia kwa Jaji Leiyla Mgonya, baada ya kuzingatia
maombi ya Kafulila aliyetaka apunguziwe gharama ya fedha za dhamana
kutoka Sh5 milioni badala yake alipe Sh1 milioni kwa kila mdaiwa.
Kupitia
Wakili wake, Emmanuel Msyani, Kafulila aliwasilisha ombi Mahakama Kuu
alipe Sh1 milioni kama dhamana kwa kila mlalamikiwa kwa kuwa hana uwezo
wa kulipa Sh15 milioni zilizotajwa kwa mujibu wa sheria ya kesi za
uchaguzi kwa mtu anayepinga matokeo.
Baada
ya uamuzi huo kutolewa, alisema anakubaliana nao na yupo tayari kulipa
kiasi hicho cha fedha ili kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani iweze
kusikilizwa na kutolewa hukumu.
Katika
maombi yaliyowasilishwa na Wakili Msyani kwa niaba ya Wakili Daniel
Lunyemela ambaye hakuwapo mahakamani, aliiomba Mahakama ikubali ombi
la mteja wake kwamba, hataweza kumudu kulipa kiasi kilichokuwa
kikitakiwa cha Sh15 milioni.
Msyani
aliiambia Mahakama kuwa kutompunguzia gharama mteja wake ni kumnyima
haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika chombo cha sheria kama
ilivyoainishwa.
Upande
wa utetezi uliowakilishwa na mawakili waandamizi wa Serikali, Juma
Masanja na Kennedy Fungamtama, waliiomba Mahakama itupilie mbali maombi
hayo kwa madai kuwa Kafulila ana mali na fedha ambazo alilipwa zaidi ya
Sh200 milioni na kwamba, alikuwa akilipwa na Bunge kila mwezi Sh11
milioni
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment