Sunday, 15 November 2015

Tagged Under:

Paris: Watu 3 wakamatwa Ubelgiji

By: Unknown On: 04:04
  • Share The Gag
  • Wakati huo huo Polisi wa Ubelgiji wamewakamata watu watatu kuhusuiana na mashambulizi hayo ya Paris yaliyosababisha vifo vya watu 129.
    Wakati huo huo Polisi wa Ubelgiji wamewakamata watu watatu kuhusuiana na mashambulizi hayo ya Paris yaliyosababisha vifo vya watu 129.
    Wizara ya sheria huko mjini Brussels eneo la Molenbeek wanasema watu hao wamekamatwa hususan kuhusiana na gari jeusi aina ya Polo lililokodishwa huko Belgium na kupatikana karibu na mojawapo ya eneo la tukio huko Paris.
    Gari hilo lilipatikana katika maeneo karibu na ukumbi wa Bataclan , 50 Boulevard Voltaire, ambapo watu 89 waliuawa baada ya wavamizi kuingia ndani ya ukumbi huo uliokuwa na mashabiki wa muziki chapa ya 'Rock' waliokuwa wanatumbuizwa na kundi la Angels of Death kutoka Marekani.
    Mmoja wa washukiwa aliyekamatwa anasemekana alikuwa Paris wakati wa mashambulio hayo Ijumaa.
    Watu 89 waliuawa baada ya wavamizi kuingia ndani ya ukumbi wa Bataclan uliokuwa na mashabiki wa muziki chapa ya 'Rock' waliokuwa wanatumbuizwa na kundi la Angels of Death kutoka Marekani. Wachunguzi hao wanasema washambuliaji hao walijipanga katika vikundi vitatu kabla ya kutekeleza mashambulizi hayo kwa mabomu na ufyatuaji wa risasi.
    Mbali na bunduki washabuliaji hao pia walikuwa na mikanda ya mabomu waliotumia kujilipua katika msururu huo wa mashambulio yaliyosababisha vifo vya watu 129.
    Ubelgiji imetangaza kupandisha viwango vyake vya tahadhari.
    Mmoja wa washukiwa aliyekamatwa anasemekana alikuwa Paris wakati wa mashambulio hayo Ijumaa. Wakati huo huo serikali ya Ugiriki imetangaza kuwa cheti cha kusafiria kilichopatikana karibu na mwili wa mtu aliyejilipua kilitumika kuingia nchini humo mwezi Oktoba na mkimbizi mmoja kutoka Syria.
    Cheti hicho cha kusafiria cha Syria kilitumika kuingia Ulaya kupitia kisiwa cha Leros karibu na mpaka wa Ugiriki na Uturuki.
    Takriban wakimbizi nusu milioni kutoka Syria waliingia Ugiriki wakitokea Uturuki mwaka huu.

    Created by BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment