Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umewataka vijana Zanzibar
kutobabaishwa na kuendelea kwa mjadala au mazungumzo ya viongozi wa
kisiasa kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu ambao
umefutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
UVCCM
imesema mazungumzo hayo ni sehemu ya harakati za kuhakikisha amani
inaendelea kuwepo nchini na kwamba hayawezi kubadilisha uamuzi wa ZEC
katika uchaguzi huo.
Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema hayo jana katika
mkutano wake na wajumbe wa umoja huo na viongozi wengine wa CCM ngazi za
kata, majimbo na wilaya kwenye ukumbi wa CCM Dimani, katika Mkoa wa
Magharibi Unguja.
Alisema
Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar ni mchakato unaosimamiwa na Sheria ya
Uchaguzi, hivyo hakuna yeyote mwenye mamlaka wala madaraka ya kuiingilia
ZEC, kuipangia au kulazimisha ipindishe sheria kwa maslahi ya wachache.
“Kukaa
kwetu kimya haimaanishi kwamba sisi si weledi wa kusema na kujipamba
kwa sifa na majigambo yasiyo na maana katika jamii, tunataka
tutofautishwe kati ya wanaojua na kuheshimu nguvu ya sheria na wale
wanaoropoka hovyo bila kujali maslahi ya nchi,” alisema.
Katibu
Mkuu huyo aliwaeleza wanachama hao wa CCM kwamba, tangu ZEC itangaze
kufuta matokeo ya uchaguzi huo, kumekuwa na kauli mbalimbali za
kibabaishaji kutoka kwa baadhi ya viongozi wa upinzani, akiwemo Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
“Hatushindwi kumjibu Maalim Seif, chama chake na wote wanaomuunga mkono, tunachelea kuonekana mbumbumbu mbele ya waelevu,” alisema Shaka.
Alisema sheria inampa mamlaka Mwenyekiti wa ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi kama alivyofanya baada ya kugundua kukiukwa kwa taratibu.
Alisema sheria inampa mamlaka Mwenyekiti wa ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi kama alivyofanya baada ya kugundua kukiukwa kwa taratibu.
Kwa
mujibu wa Shaka, baada ya uamuzi huo anaepita mitaani na kusema
anasubiri aapishwe awe Rais wa Zazibar wakati Ikulu ipo chini ya rais
halali kisheria, huyo anaota mchana na anajiweka wazi jinsi alivyo na
uchu wa madaraka.
Aidha,
alisema mivutano itokanayo na utata wa kisheria haitamalizwa na vinywa
vya wanasiasa wenye tabia ya kukanyaga sheria au kubeza matakwa ya
katiba. Kwa mujibu wa shaka, sehemu yoyote inayohitaji msaada wa
mazungumzo, ni jambo la kawaida kwa wanasiasa na viongozi kukutana,
ingawa hatua hiyo haihalalishi kuvunjwa kwa sheria na katiba ya nchi.
Shaka
alisema uendeshaji wa nchi yoyote duniani, husimamiwa na kulindwa
kisheria na katiba, hivyo kinaweza kuwa kituko iwapo mwanasiasa atadhani
kwa kushinikiza jambo, anaweza kupewa nafasi ya uongozi wa juu wa nchi.
“Iwapo
ZEC imefuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu kutokana na uwezo wa kisheria
walionao, sasa ni wajibu wao tena kuwaeleza wananchi ni lini watapiga
kura tena, ili watimize haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa
kidemokrasia,” alisisitiza.
Aliwataka
vijana wa CCM kuwa makini, wavumilivu na wenye ari ya kudumisha
mapinduzi yao, huku akiwataka kusahau wale wote wenye mawazo ya kutaka
kuyazika kwa kuwa hilo halitawezekana milele.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment