Wakati Serikali ikikunjua makucha yake dhidi ya wote waliohusika katika kashfa ya kupitisha makontena 349 kwenye Bandari ya Dar es Salaam bila ya kuyalipia kodi, imefahamika kuwa idadi hiyo ya makontena ni sehemu ndogo tu ya mamia ya mizigo yanayovushwa kinyemela kila uchao na kuikosesha serikali mabilioni ya fedha.
Hata
hivyo, wakati serikali ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake, Kassim
Majaliwa, ikiendelea kutafuta suluhu ya kudumu kuhusiana na ukwepaji
kodi, imebainika kuwa kazi hiyo siyo lelemama kwani zipo njia zaidi ya
tisa zinazotumiwa kukwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mosi, ni kupitia mwanya utokanao na mfumo wa zamani wa malipo usiohusisha ule wa sasa wa kielektroniki, maarufu kama ‘E-Payment’.
Kwamba, wafanyabiashara wengi hutumia mfumo huo wa zamani unaohusisha matumizi ya karatasi zilizojazwa kwa mkono na hivyo kuwezesha ujanja wa kubadili taarifa kwa manufaa ya mitandao ya wakwepaji wa kodi.
Kwamba, wafanyabiashara wengi hutumia mfumo huo wa zamani unaohusisha matumizi ya karatasi zilizojazwa kwa mkono na hivyo kuwezesha ujanja wa kubadili taarifa kwa manufaa ya mitandao ya wakwepaji wa kodi.
“Tatizo
lililopo ni kwamba mfumo wa E-Payment ni mpya (umeanza Julai) na
umefungwa kwenye benki moja tu iliyopo ndani ya eneo la Bandari… ule wa
zamani unaendelea kutumiwa na wajanja hucheza na maandishi ya kujaza kwa
mkono kuhujumu mapato ya serikali,” chanzo kimeeleza.
Njia ya pili
ya kuhujumu mapato bandarini hapo, imetajwa kuwa ni ya kushirikiana na
maafisa wa benki. Hii ina uhusiano mkubwa na njia ya kwanza inayohusisha
matumizi ya mfumo wa malipo wa zamani usiokuwa wa kielektroniki.
Mfanyabiashara anaweza kuandikiwa kodi sahihi anayotakiwa kulipa, lakini anashirikiana na wafanyakazi wa benki anayokwenda kuweka fedha kwa kuhakikisha kuwa baada ya kufanikiwa kuondoa kontena bandarini, maafisa wa benki husika husitisha malipo hayo kwa kuondoa fedha husika kwa madai kuwa fedha ziliingizwa kwenye akaunti husika kimakosa.
Mfanyabiashara anaweza kuandikiwa kodi sahihi anayotakiwa kulipa, lakini anashirikiana na wafanyakazi wa benki anayokwenda kuweka fedha kwa kuhakikisha kuwa baada ya kufanikiwa kuondoa kontena bandarini, maafisa wa benki husika husitisha malipo hayo kwa kuondoa fedha husika kwa madai kuwa fedha ziliingizwa kwenye akaunti husika kimakosa.
“Huwa
kuna ushirikiano wa karibu kati ya maafisa wa benki na mfanyabiashara
husika. Baada ya kontena kutolewa bandarini, hamisho la fedha
(transaction) huondolewa katika mfumo kwa maelezo kuwa halikuwa sahihi,”
chanzo kimedai, huku kikisisitiza kuwa ushirikiano huo huhusisha
pia watu wa Bandari na TRA ambao mwishowe hugawana malipo kadri
wanavyokubaliana.
Tatu, ni
mwanya wa uvushaji wa makontena yenyewe yasiyolipiwa ushuru kupitia
mageti maalum yanayofahamika kwa kazi hiyo, hasa geti Namba 3 ambalo
chanzo kimedai ndilo linaongoza kupitisha mizigo ya ‘dili’.
“Kwa ujumla yapo mageti matano ya kupitisha bidhaa mbalimbali, baadhi yakiwa ni ya kupitihia mafuta, nafaka na magari.
"Hili Namba 3 ndiyo hutumika kupitisha makontena ya bidhaa zenye thamani kubwa na wengi wasiolipa kodi hulitumia hili,” chanzo kilieleza kabla ya kufafanua kuwa awali, hilo geti Namba 3 halikuwa na mfumo wowote wa kuangalia kama kontena husika limelipiwa au la na ndiyo maana lilikuwa likitumika zaidi kupitisha makontena yasiyolipiwa kodi.
"Hili Namba 3 ndiyo hutumika kupitisha makontena ya bidhaa zenye thamani kubwa na wengi wasiolipa kodi hulitumia hili,” chanzo kilieleza kabla ya kufafanua kuwa awali, hilo geti Namba 3 halikuwa na mfumo wowote wa kuangalia kama kontena husika limelipiwa au la na ndiyo maana lilikuwa likitumika zaidi kupitisha makontena yasiyolipiwa kodi.
Njia ya nne
ya kuhujumu kodi ya mapato ni ya kuwatumia watu wanaoendesha bandari
kavu (ICD’s). Inaelezwa kuwa hivi sasa kuna bandari kavu 12, ambazo kila
meli inapoingia hujulikana kila mzigo husika unapelekwa kwenye bandari
ipi kati ya hizo.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kinachofanyika ni kwa baadhi ya makontena yanayotolewa bandarini ili yapelekwe bandari kavu kabla ya kukombolewa na wahusika huishia kupelekwa kwa wafanyabiashara wenye makontena na hivyo kuikosesha mapato serikali.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kinachofanyika ni kwa baadhi ya makontena yanayotolewa bandarini ili yapelekwe bandari kavu kabla ya kukombolewa na wahusika huishia kupelekwa kwa wafanyabiashara wenye makontena na hivyo kuikosesha mapato serikali.
“Awali
kwenye ICD’s kulikuwa na askari wa mmiliki wa ICD’s na siyo wa TPA…
huyu alikuwa akiangalia malipo ya bosi wake tu ambayo ni gharama za
kuhifadhi mzigo na hivyo TPA na TRA huambulia patupu,” chanzi
kimeeleza, kikiongeza kuwa hivi sasa walau kuna nafuu kwani kwenye ICD’s
kuna walinzi wa TPA lakini hilo limefanyika baada ya watu kuwa tayari
wameshaiba sana.
Njia ya tano inayotumiwa
kukwepa kodi ni ya kubadili taarifa, hasa kupitia watu wenye wajibu wa
kufanya tathmini. Kwamba, badala ya mzigo kukadirwaa kodi kwa kiwango
sahihi, wahusika ambao zaidi huwa ni watu wa TRA hukadiria fedha kidogo
baada ya kujihakikishia kuwa nao wanapewa mgawo na wafanyabiashara.
“Hapo
utakuta kontena la kodi ya milioni 80, mteja anaambiwa alipe milioni 40
tu … na wakati mwingine kiasi hicho pia hakiandikwi balki huandikwa cha
chini zaidi kama milioni 5 tu…hii ni njia nyingine inayoligharimu taifa
mabilioni ya fedha,” chanzo kimeeleza.
Njia ya sita
inayofanikisha ukwepaji kodi ni mtandao mpana wa baadhi ya vigogo wa
maeneo mbalimbali Bandarini na TRA, ambao hawa huhakikisha kuwa wanakuwa
na timu ya vijana wao wa kazi karibu katika kila eneo ili kufanikisha
mipango yao.
“Hii
ndiyo njia kubwa ya hujuma. Kama utakumbuka aliyekuwa Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alisambaratisha baadhi ya mitandao kwa
kuwagusa vigogo 27… ile ilikuwa kuvunja mtandao uliokuwapo. Hilo
lilisaidia kiasi, lakini sasa ipo pia mitandao mingine ambayo uchunguzi
ukifanyika utabaini kuwa mambo yameanza kurudi kama zamani,” imeelezwa.
Njia ya saba
ya ukwepaji kodi ni kwa baadhi ya vigogo wa Bandari na TRA kuanzisha
kampuni zao za uondoaji mizigo bandarini. Inaelezwa kuwa hizi hutumiwa
sana kufanikisha ‘dili’ za ukwepaji kodi na ndiyo maana haishangazi
kusikia kuwa kuna makontena zaidi ya 300 hayaonekani kwenye kumbukumbu
za TRA.
Njia ya nane
ya ukwepaji kodi ni kuonyesha kuwa kontena linapelekwa nje ya nchi, kwa
mfano Malawi, wakati ukweli ni kwamba huishia hapahapa nchini.
“Utakuta
kontena linadaiwa kupelekwa Malawi, lakini linachukuliwa na gari kukuu
linaloonekana wazi kuwa haliwezi kufika hata Kibaha… njia hii pia
hutumiwa sana kuikosesha serikali mapato,” chanzo kingine kilisema
Njia ya tisa
ya ukwepaji kodi ni ucheleweshaji wa makusudi wa utoaji makontena.
Kwamba, mteja anapotaka kutoa mzigo wake kwa kufuata njia halali
zilizopo, huishia kuzungushwa kila uchao ili akubali kutoa rushwa na
mwishowe kulipishwa kiwango pungufu cha kodi au kulipa fedha zisizoingia
kabisa kwenye mikono ya TRA.
Njia ya kumi
ni ubabaishaji unaofanyika katika kuorodhesha idadi ya makontena
inayotolewa bandarini kwenda kwenye bandari kavu. Hapa, kama makontena
yanayotolewa ni 12, basi huandikwa kuwa ni 10 na mengine mawili huishia
kuondolewa bila ya kuwa na kumbukumbu zake kwa ajili ya kulipiwa kodi.
Pamoja
na kuwapo kwa njia zote hizo, chanzo kimedai kuwa sababu kubwa ya
kufanikiwa kwa ukwepaji kodi ni mtandao mpana unaoundwa na vigogo
mbalimbali na ndiyo maana taarifa mbalimbali za wakaguzi wa ndani na wa
nje katika Bandari ya Dar es Salaam huishia kubaki kwenye makabrasha
bila ya kuwapo kwa utekelezaji wowote wa vitendo juu ya yale
yanayopendekezwa na wataalamu.
Chanzo: Nipashe
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment